SportsHistoria

Mengi kuhusu historia ya Simba na yanga

Kama utakuwa wapenda soka na unaishi nchini Tanzania, basi utakuwa unaelewa machache kuhusu Simba na yanga. Nataka Leo nichukue fursa hii kuwajulisha Mengi kuhusu historia ya Simba na yanga.

Historia ya Simba na yanga

Ningependa sana utakapo ipokea hii historia ya Simba na yanga, uweze ku share na wenzako maana wengi wamekuwa wakiulizana kuhusu Simba na yanga Ila hawajaifahamu historia vizuri.

Picha za Yanga fc

Timu ya yanga imekuwepo kwa mda na haikuanzishwa juzi kama unavyodhania. Yanga ni timu mojawapo ya zile klabu za zamani nchini Tanzania. Yanga ilianzishwa mwaka wa 1935. Najua Jambo hili limekushangaza Ila kwa sasa Yanga imekuweko kwa zaidi ya miaka sabini.

Yanga ilianzishwa hata kabla ya Simba Ila hazijaachana sana kwani timu ya Simba nayo ilianzishwa mwaka uliyofuatia baada ya yanga. Timu ya Simba ilianzishwa mwaka wa 1936.

picha za Simba

Timu hizi mbili zinapendwa sana na watu wengi tangu kuanzishwa kwake na kwa sababu ya mapenzi ya mashabiki wao, kumekuwa na upinzani mkali sana Kati ya wafuasi wao. Yanga na Simba wakiwa uwanjani, mashabiki hujitokeza sana na sio wengi hupenda kukosa mechi za timu hizi mbili.

Upinzani wao ulianza hizi timu zikiwa bado hazijahitimu kuwa za kitaifa. Kumbuka timu hizi zilianzia mitaani na hapo ndipo mashabiki walijigawanya vikundi vikundi kila shabiki akitoa sapoti kwa timu yake anayoipenda. Baada ya mda, Simba na yanga walijulikana kimataifa na kwa sasa wako na mashabiki wa taifa nzima la Tanzania. Hii Ina maana kuwa upinzani umeongezeka nchi nzima na hata afrika kwa jumla.

Tangu kuanzishwa kwa yanga na Simba, wamekutana zaidi ya Mara 84. Kulingana na utafiti wetu, timu ya yanga imeishinda Simba Mara nyingi japo wawili hawa wanapimana nguvu. Wakati mwingine timu hizi huenda sare na hii inaonyesha wazi kwamba, kila timu Ina bidii.

Takwimu zetu zaonyesha kwamba, yanga imeshinda Mara 31 na Simba nayo imeshinda Mara 24 huku wakienda sare Mara 28.

Yanga kwa sasa imefunga simba zaidi magoli 112 na Simba imefunga yanga magoli 91

Mechi za historia Kati ya Simba na yanga

Simba na yanga live

Kuna mechi moja ya yanga na Simba itabaki kuwa historia. Hii ilikuwa mwaka wa 1977. Simba ilimfunga yanga magoli 6 kwa nunge. Simba haikukomea hapo kwani mwaka wa 2012 iliifunga tena yanga 5-0.

Tangu kuanzishwa kwa timu hizi mbili, yanga imeshinda ligi kuu Mara ishirini na saba huku Simba ikishinda Mara kumi na tisa.

Kwa sasa tunakomea hapo hapa mwangaza news na bila shaka umefahamu Mengi kuhusu historia ya Simba na yanga. Ningependa uchukue nafasi hii ku share na wenzako pia wafahamu pia mengi zaidi kuhusiana na timu ya yanga na Simba.

Soma hii pia : TRA huduma kwa wateja na TIN namba

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *