MchipukoSiasa

Murkomen na Susan Kihika wapoteza nafasi zao katika bunge la seneta

Baada ya vuta nikuvute, Murkomen na Susan Kihika wamepoteza nafasi zao katika bunge la seneta. Wawili hao ni wanachama wa jubilee na kwanzia Sasa hawatakuwa wakipata marurupu yao Waliokuwa wakipata.

Siku ya jumatatu, wawili Hawa waling’atuliwa na hapo kwa hapo nafasi zao zikachukuliwa. Mkutano wa kuwatoa kwa nafasi zao iliongozwa na rais Uhuru Kenyatta. Kiongozi wa wengi bungeni Mr kipchumba Murkomen na Susan Kihika waliacha nafasi zao zilizochukuliwa na senator Samuel poghisio wa west pokot na nafasi ya Susan Kihika ikachukuliwa na seneta wa murang’a Irungu Kang’ata.

Murkomen na Susan Kihika nje ya Bunge
Murkomen na Susan Kihika nje ya Bunge

Huenda wawili hao wakapoteza nafasi zao za ofisi pia. Waliochukua nafasi Sasa wameanza kazi Mara moja na huenda wakalipwa zaidi hata kuliko Murkomen na Susan Kihika. Habari zingine zaongezea kuwa wawili hao waliochukuwa hizo nafasi wameongezwa ulinzi.

Kulingana na John Mbadi, kiongozi wa wachache bungeni, Vyeo walivyopoteza Murkomen na Susan Kihika hupokea zaidi ya laki mbili na nyongeza za hapa na pale zenye pia ni zadi ya laki moja na ishirini. Hii Ina maana ukiwa kwa nafasi hii unapokea laki nne zaidi ya seneta wengine.

Pia soma (Utajiri wa Raila Odinga)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *