Sanaa

Mzee Yusuf kurudi kwenye mziki

Kama umekuwa ukifuatilia Sanaa ya nchini Tanzania Basi bila shaka unamfahamu mzee Yusuf. Ni msanii aliyejulikana sana Kama bingwa wa mziki wa taarab. Miaka Kama tatu iliyopita aliweza kutangaza rasmi kwamba kaacha mziki wa taarab na kuamua kumrudia Allah.

Amekuwa mafichoni kwa mda Sasa na iliwahi kusemekana alipipitia magumu sana baada ya kuacha mziki ikizingatiwa kuwa ako na Bibi zaidi ya mmoja na wote wanahitaji kulishwa. Hivi maajuzi aliweza kusema kuwa atarudi mjini Kama ilivyokuwa hapo awali. Kulingana na habari za kuaminika, gwiji huyu wa mziki wa taarab inasemekana anataka kurudi kwa Sanaa ya mziki.

soma hapa (Alikiba na Hamisa Mobetto waumiza diamond)

Kile hakijajulikana kabisa ni je, ataka Rudi kwa mziki wa taarab ama qaswida?. Swali nyeti Ila mwenyewe kasema atatangaza rasmi kwa hivyo watu wazidi kuwa na subra kwani anachotaka kifanya amekiwaza kwa mda na hivi Sasa amefanya maamuzi yake na kuamua kufanya anachokitaka.

Letu jicho tu Ila tukizipata taarifa zaidi kuhusu mzee Yusuf Basi utakuwa wa kwanza kuzipokea. Asante sana kwa kuwa nasi ndani ya Mwangaza

Tazama video yake Mpenzi chocolate 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *