Mchipuko

Nadia Mukami na Arrow Bwoy wamkaribisha mtoto wao wa kwanza

Ni furaha kwa wawili hawa baada ya kupata mtoto wao wa kwanza. Nadia Mukami na Arrow Bwoy wamekuwa kwenye uhusiano kwa mda sasa na bilashaka matunda yameanza kuonekana.

Habari ya kuzaliwa kwa mwanao iliwekwa wazi kwenye mitandao huku wakipachika picha kwenye Instagram. Kulingana na arrow Bwoy, wawili hawa wamebarikiwa na mtoto wa kiume na mtoto na mama wako salama na afya tele.

Kwa upande wake Nadia Mukami alionekana mwenye furaha na kwenye Instagram yake aliandika ujumbe wa kumsifia mwanawe wa kiume waliompa jina la Haseeb Kai. Hichi ndicho alichokiandika kwa page yake ya Instagram

Arrow Bwoy child

“24.03.2022 We received the most Beautiful Gift Ever @haseebkai welcome to our world @nadia_mukami thank you @rfh_healthcare my Queen and the Prince are in the safe hands. Welcome to our World Haseeb Kai @haseebkai. 24th March 2022.”

Wakenya nao hawakuachwa nyuma kwa kuwapongeza wawili hawa kwa hatua ya maisha waliyoipiga.

“Congratulations my brother n my sister,” wrote KRG the Don.

@prezzo254: “Congratulations brother God bless u & ur family.”

@michelle.ntalami: “Congratulations guys!

@badgyalcecile: congrats my brother to you and the family”

@dkkwenyebeat: “Congratulations

@massawejapanni: “Dadangu mdogo Karibu kwa uzazi! Kweli utapenda

Nadia Mukami na Arrow Bwoy walianza uhusiano wao mwaka mmoja uliopita. Ilianza na colabo waliyoifanya na kwenye video walionekana na ukaribu mkubwa sana.

Nadia Mukami child

Safari ya Nadia ya ujauzito imekuwa tofauti sana kwani aliamua kuieka Siri. Nakumbuka kuna wakati jalango alijikuta taabani kwa kutangaza wawili hao wanatarajia mtoto. Nadia Mukami hakufurahishwa na jambo Hilo kwani alikuwa yuataka iwe Siri. Ni juzi tu alijitokeza na kutangaza ujauzito wake wiki mbili kabla hajazaa.

Hapa mwangaza news tunawatakia maisha marefu wawili hawa na afya tele kwao pamoja na mtoto wao Haseeb Kai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *