AfyaMchipuko

Naibu wa Gavana wa kilifi county aomba msamaha

Hakuna binadamu aliyekamilika na wakati mwingine binadamu hufanya Jambo likaweza kuwakwaza wengine au kuadhiri hata bila kukusudia. Naibu Gavana wa kilifi Gideon Saburi ajikuta pabaya baada ya kusambaza virusi vya Coronavirus bila kujua.

Inasemekana kuwa alikiuka amri ya kutojitenga na watu alipotoka ujerumani na hivo kuwa chanzo Cha virusi hivyo county ya kilifi. Kwa Sasa naibu huyo wa Gavana ako hospitali ya mkoa wa pwani inayojulikana Kama coast general.

Gideon Saburi jana aliweza kuomba wanainchi watufu waweze kumsamehe kwa makosa yake huku akiongezea kuwa hakukusudia kwani yeye anajali binadamu wenzake ikifahamika kuwa pia yeye ana familia na anajali masilahi ya kila mtu.

Kwa Sasa Coronavirus imechangikia marufuku ya wakenya kutotoka nje baada ya saa moja usiku ili serikali iweze kukabiliana na homa hiyo hatari. Kwa Sasa, Kenya ina Zaidi ya kesi thelathini za virusi vya Coronavirus.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *