MaishaMchipuko

Nilimtuma rafiki yangu amjaribu mume wangu sasa wameoana

Mitandao hutumiwa na wengi ulimwengu mzima. Kuna wengi walipatana kwenye mitandao na kwa sasa wameoana. Wengi hutumia mitandao kutangaza biashara zao ila wengine hutumia kwa kueleza maisha yao na wakati mwingine kueleza masikitiko yao. Hii ina maana kwa mitandao huenda ukapata kila aina ya maneno kutoka kwa watu.

Juzi msichana mmoja kutoka nchini Nigeria aliweza kueleza masikitiko yake kuhusiana na mapenzi kati yake na aliyekuwa mpenzie. Pearl alisema walipanga na rafiki yake ili amjaribu mchumba wake ndio ajue anampenda kiasi gani na kama ana mchepuko. Cha ajabu ni kuwa aliyetumwa ni kama alikuwa anangojea hiyo nafasi kwani mambo hayakwenda kama alivyopanga Pearl.

Inaonekana hili lilifanyika mda mrefu uliopita ila machungu ya Pearly yamemfanya kuelezea uma baada ya mda mrefu kupita. Kulingana na pearl Wawili hawa, rafiki ya pearly na Mchumba wa pearly walioana na sasa wako na watoto wawili.

Miaka mitano iliyopita, niliweza kupanga na rafiki yangu akamjaribu mchumba wangu ili nijue kama ananipenda, nasikitika kwani sasa wameoana na hivi wana watoto wawili. Anita mungu atakusamehe kwa niaba yangu.. …Ndivyo alivyoandika kwa ukurasa wake wa twitter

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *