Mchipuko

Nyani zajazana maeneo ya Thailand kwa kukosa lishe kutokana na Coronavirus

Nyani nchini Thailand walishindwa kuvumilia na kuamua kuvamia miji mikuu ya nchi hiyo. Nyani hao wamekuwa wakipokea chakula kutokana na uwepo wa watalii. Kutokana na virusi hatari vya Coronavirus, nyani hao wamekosa msaada kwani watalii wamepungua nchini humo.

Inasemekana nyani hao wanatembea kwa pamoja na imefikia hatua hata wanaweza kumpokonya binadamu chakula wakikutana naye njiani. Coronavirus imeadhiri nchi nyingi kwa Sasa na huenda uchumi ulimwengu mzima ukaenda chini kwani biashara nyingi zimesimama.

Sekta ya utalii imeadhirika pakubwa mno kwani nchi nyingi zimepiga marufuku usafiri wa kutoka ama kuingia nchi nyingine. Sekta ya utalii hunufaisha nchi nyingi sana na mabilioni ya pesa hupatikana kupitia utalii.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *