MaishaMchipuko

Nyumba ya Zuchu yazua gumzo

Habari zinazotufikia ni kwamba nyumba ya Zuchu ipo tayari na kwa sasa anaweza kuishi. Ni nyumba kubwa sana na huenda akahamia hapo na familia nzima kwani itakuwa vigumu kuishi peke yake ikizingatiwa kwamba bado hajaoleka.

Zuchu alionyesha mjengo wake wa mamilioni ya pesa na kusema ana furaha isio na kifani kwani amekuwa kwa Sanaa ya mziki kwa mwaka mmoja tu na tayari anaona mafanikio yake.

Zuchu alipakia video kwenye mtandao wake wa Instagram huku akionyesha nyumba yake iliyoko nchini tanzania na kuipa jina la white house. Nyumba ya Zuchu Ina gorofa mbili na inaonekana kuwa ya kisasa zaidi.

Nyumba ya Zuchu yazua gumzo

Kwenye gorofa la pili Kuna balcony inayotazama main gate. Sababu ya Zuchu ku post video ya nyumba yake ilikuwa kuwapa Moyo wenzake waonafanya bidii na kuwataka kutokata tamaa kwani siku yao ya mafanikio yaja. Nyumba ya Zuchu inaonyesha wazi kwamba bidii yalipa.

Zuchu ambaye sasa ni malkia wa bongo amekuwa akifanya Kazi na diamond platnumz kwenye label ya wasafi miezi 17 iliyopita. Tokea mda huo maisha ya Zuchu yameimalika na anaonekana kufanikiwa zaidi.

Wengi walikutana na video inayoonyesha nyumba yake kwenye Instagram stories siku ya jumatatu tarehe 6 September. Nyumba yenyewe ameibandika jina la white house kwani anadai inafanana na ikulu ya marekani anapokaa Rais joe Biden.

Imezungushwa ukuta mzuri na gate ya rangi nyeusi ambapo unaweza kuitazama nyumba hiyo ukiwa nje ya gate. Kwenye hiyo video zuchu aliandika haya,

” Nashukuru Mungu kwa zawadi hii aliyonipa na pia siwezi wasahau mashabiki wangu kwa sapoti yenu na ningependa kuhimiza kila mmoja kutokata tamaa.. Mungu ni mwaminifu kwani amenitendea mengi kwa mda wa mwaka mmoja….”

Ni miezi kadhaa iliyopita ambapo zuchu pia alimzawadia mamake khadija kopa gari la kifahari. Kulingana na Zuchu kabla ya kumununulia mamake gari, zuchu alikuwa akifuatilia ni gari gani mamake alikuwa akitamani maishani mwake na baada ya kupata jibu alimunulia gari ambayo ni Toyota Alphard.

Mamake alifurahi sana kwa hiyo zawadi kutoka kwa mwanawe zuchu huku akimuombea mungu azidi kufanikiwa zaidi. Zuchu alisema kwamba ana furaha kumununulia mamake gari kwani Kuna wakati alikuwa hana uwezo wa kumlipia mamake nauli ya matatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *