MchipukoSiasa

Oscar Sudi ajipata matatani kuhusiana na kifo Cha Chris Msando

Akiongea na wanahabari, Oscar Sudi alidai kuwa atawataja walio ua Chris Msando. Sudi aliongeza kuwa wafuasi wa naibu wa rais William Ruto wanafuatwa futwa na watu wasiojulikana huku akisema wanatishiwa kwa mkondo waliochukua wakisiasa.

Oscar Sudi alisema hatawatishika kivyovyote vile. Mbunge wa Alego Samuel Atandi alimuomba George Kinoti ambaye ni mkurugenzi wa kitengo Cha criminal investigation kumfungulia mashtaka Oscar Sudi kuhusiana na kifo Cha Chris Msando.

Jumamosi iliyopita akiwa pamoja na Mp wa bahati Kimani Ngunjiri, walisema siku ikifika watawataja walio ua Chris Msando

Atandi mwenye pia ni mkaribu wa naibu wa rais alisema kwamba kifo Cha msando hakifai kutumika Kama silaha kwenye siasa. Alisema kuwa Sudi anafaa kushtakiwa Mara moja kwani familia ya Chris Msando imekuwa ikitafuta aliyemuua kwa mda mrefu.

Akiongea na wanahabari wa nation Media kwa njia ya simu, Atandi aliseme Oscar Sudi anafaa kushikwa ili asaidie kutafuta walioua Chris Msando.

Soma hii pia ( Huenda Uhuru akamtaja Raila kama Mrithi wake )

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *