Sanaa

Otile Brown na vera Sidika waanzisha Vita

Kama una kumbukumbu, Vera Sidika na Otile Brown waliwahi kugonga vyombo vya habari kwa uhusiano wao wa kivyake. Kwa sasa uhusiano wao haupo tena ila kila uchaoni lawama kwa kila pande.

kwa sasa wawili hao hawa wanarushiana maneno waziwazi na hata kuongelea Siri zao za kindani. Yaonekana kila mtu ana machungu na mwenzake ndio maana kila mtu anatetea upande wake.

Vera Sidika aliwahi kusema uhusiano wao hauchukua hatua yoyote na alidai kuwa kuna mambo hayakumfurahisha kuhusiana na Otile Brown.

Vera Sidika alisema Otile Brown anapenda kuombaomba sana. Aliwahi kumpa laki tano bila kusahau alimnunulia Mercedes Benz mpya.

“Hata Kama sisi wanawake tukipenda tunapenda kweli, mwanaume akianza kuitisha pesa huwa tunalemewa. Mwanaume hafai kumtegemea kihela mwanamke. Kuna wakati huwa tunafaa kusaidiana lakini haifai kila Mara mwanaume anaomba pesa

“.. Baada ya kuwa na uhusiano na Otile Brown, alianza kuitisha pesa kwangu akiahidi kuregesha lakini hakuwahi. Mimi sikuwahi kumuomba pesa hata siku moja ila kwake ilikuwa tabia ya kila siku. Hapo ndipo nikaelewa kuwa hakuwa na mapenzi kwangu ila alichokitaka kwangu ni pesa tu. Wakati Otile Brown alinikopa laki tano nikasema sina, alininyamazia kwa mda wa wiki moja. Baadae alijitokeza na kuniambia kuwa uhusiano wetu huwezi endelea…”

Otile Brown na vera Sidika

Vera Sidika alisema hawezi kubali kutumika kihela. Vera beauty parlour iliwahi kusaidia Otile kwa malipo ya studio na pia usafiri wa ndege.

Kwa kujitetea kwake, Otile Brown alikanusha madai hayo na kusema hiyo Deni alichukua lakini alikuwa alipe baadae. Alisema Vera Sidika ana aibu ndogo ndogo kwani kila mtu alikuwa anaomba pesa kwa mwenzake.

Otile Brown aliongeza na kusema ashalipa Deni ya vera Sidika. Otile alidai kuwa uhusiano wao haukukatika kwa sababu ya pesa ila Vera Sidika alitaka kuolewa na wazae watoto. Vera Sidika naye akijibu na kusema hajawahi kuitisha Otile Brown pesa.

Soma hii pia ( utajiri wa harmonize)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *