Mchipuko

Papa Shirandula ( Charles Bukeko afariki

Papa Shirandula ambaye jina lake kamili ni Charles Bukeko ameaga dunia. Papa Shirandula ni muigizaji na kabla ya kupatana na mauti, alikuwa anaigiza ndani ya citizen Tv, tamthilia kwa jina papa Shirandula.

Wakitangaza kifo chake, familia yake ilisema kuwa papa Shirandula aliaga dunia  jumamosi asubuhi baada ya kuugua kwa mda mfupi. Alikuwa ni mtoto wa kwanza kwa familia na ameaga dunia akiwa na miaka 58.

Papa Shirandula ashawahi kupata tuzo kalasha awards mwaka wa 2010 kama muigazi Bora wa runinga. Amemuacha mke mmoja Beatrice Ebhie Andega na watoto watatu, Tony, charlie na Wendy

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponiPapa Shirandula

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *