Sanaa

Hii ndio hela anayolipwa MCA Tricky

 

MCA Tricky ni mmoja Kati ya wachekeshaji wanaopendwa zaidi nchini Keanya. Akisimama kwa jukwa huwa ana wacha watu vinywa wazi kwa vichekesho vyake. Yeye hujitambulisha Kama mmoja wa kikundi Cha wanachokora.

MCA Tricky jina lake kamili ni Paul kimani njoroge. Tangu ajiunge na Churchill show, mchekeshaji huyu Hana upinzani wowote na tokea mwaka wa 2016 bado anaonekana kukomaa kwa vichekesho na anazidi kuwa mkali zaidi.

Tofauti yake haswa huwa talanta yake ni ya kukua nayo na huwa sio mtu wa kuiga hivyo kubakia bila upinzani. MCA Tricky alisoma mpaka darasa la nane. Kutosoma kwake hadi shule ya upili ama chuo kikuu, hakukumzuia kuwa kwa kikundi kimoja na akina Hamo, jesee na wengine wengi.

MCA Tricky amezaliwa kwenye familia maskini na hii ndio sababu hakuweza kujiunga na chuo Cha pili kwani familia yake haikupata ada ya shule iliyokuwa yahitajika. Yeye ni mdogo katika familia yake ambapo wako watatu. Mchekeshaji huyu anasema aliingia katika kikosi Cha chokora huko Nairobi bila wazazi wake kujua.
MCA Tricky na mpenzi wake Rue baby akothee

MCA Tricky amezaliwa makindu na yeye kwenda Nairobi halikuwa wazo lake Ila marafiki zake walimhimiza kuwa Nairobi atapata kazi nzuri na hapo ndipo akaamua kwenda. Kufika Nairobi akagundua kuwa maisha ya huko ni magumu hata kuliko kwao makindu na hata kutaka kurudi kwao.

Mda flani, MCA Tricky alipata kwa kuishi Ila msamaria mwema aliyempa hiyo nafasi alikuja kumfukuza siku moja na kubaki hana kwa kwenda. Hapo ndio akaingia kwa street na kuanza maisha ya uchokora.

MCA Tricky anawashukuru sana Barikiwa set book group kwani wao ndi walimfungulia njia. Kwa bahati nzuri kikundi hichi kilipendezwa na uchekeshaji wake na wakaamua kumsaidia

Akiwa kwenye barikiwa set book group, MCA Tricky alipata sapoti kubwa sana na wengi wakamhimiza ajiunge na Churchill. Kwa bahati nzuri, siku moja Churchill aliandaa show yake carnivore ground ambapo pia alikuwa yuatafuta wachekeshaji wapya. Hapo Churchill, MCA tricky aliwapata akina pro. Hammo na walizidi kumpa moyo zaidi.

Ni juzi tu Daniel ndambuki aliweza kugonga vyombo vya habari huku wengi wakidai hajawalipa wafanyi kazi wake. Bingwa huyu ni kiongozi wa show mbili ambazo ni Churchill Raw na Churchill live.

Akijibu mashtaka hayo, Daniel ndambuki alisema mbali na malipo, Churchill show inalea vipaji. Aliongezea na kusema Kama mtu anaingia Churchill show na malengo ya pesa Basi ataumia Ila Kama anaingia Churchill kukuza talanta yake, Basi atafanikiwa sana maishani. Alisema mambo ya pesa sio ya kuongelewa hadharani Ila watu waangalie walipofikia tangu wajiunge na Churchill show.

MCA Tricky graduation

Hii ndio pesa MCA Tricky analipwa kwa show moja

Anaonekana analipwa vizuri, Kulingana na mahojiano tofauti tofauti,
MCA Tricky alidai huwa anachukua millioni ila kwa Churchill show inasemekana analipwa ksh.150,000 per month

MCA Tricky bado ni mtangazaji radio maisha ambapo yeye huingia asubuhi kwenye breakfast show wakiwa na Billy Mia.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *