Maisha

Picha ya Lilian Nganga yazua utata

Lilian Nganga amekuwa akigonga vichwa vya habari kwa mda sasa baada ya kusema kwamba aliyekuwa mumewe amekuwa akimtishia.

Baada ya ku post picha yake huku akionekana mwenye tabasamu, wakenya wengi waligundua  kuwa Kuna tatizo flani anayoipitia kwani mwili wake unaonekana kupungua.

Lilian Nganga photos

Kutoka aachane na Alfred Mutua na kuanza maisha mapya na Juliana, Lilian Nganga amekuwa akifuatiliwa sana na wengi ili kujua anavyoendelea.

Baada ya ku post hiyo picha, wengi walianza kurusha comments za kila aina. Asilimia zaidi ya sabini wailikuwa wakiongelea mwili wake kuonekana kupungua.

Lilian Nganga Instagram

Japo wengi waliona anapitia wakati mgumu na ndio maana amepungua, kunao pia waliomtetea huku wakisifu muonekano wake mpya  wakidai mwili mdogo huashiria afya.

Walipoacha na gavana wa machokos mheshimiwa Alfred Mutua, Lilian alidai kwamba Mutua hataki kabisa kumuachilia Lilian huku akisema Mutua ameanza kufuata Mali yake kama gari na vitu vingineo.

Lilian alisema kuwa ameripoti Mutua na kesi yao ipo kortini huku akidai ana stakabadhi zote zakuonyesha kwamba, Mali anayoitaka Mutua ni yake.

Hapa mwangaza tuna matumaini kwamba Lilian Nganga ako salama na kupungua kwa mwili wake hakumanishi anapitia wakati mgumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *