Sanaa

Picha za Jihan Dimack mpenzi mpya wa diamond platnumz

Jihan Dimack alijitokeza kwa show ya Zuchu akiwa amevalia vazi lililofana na vazi la diamond platnumz. Hii ni katika Sherehe ya Zuchu iliyofanyika tarehe kumi na nane july.

Mndani mmoja wa WCB amehakikishia watu kwenye mitandao kuwa kweli jihan Dimack ni mpenzi wa diamond na hivi karibuni wawili hawa watafunga ndoa.

miss universe Tanzania

Tarehe 18 July diamond platnumz aliandaa tanasha ya kumkaribisha rasmi zuhura kopa anayejulikana kama Zuchu kwenye wcb. Kwa sasa wasafi iko na wasanii watano akiwemo diamond platnumz. Wasanii hawa ni Lavalava, Mbosso, Rayvanny, Zuchu na diamond platnumz ambaye ndiye kinara wao.

Kabla ya jisaa limoja ndio tamasha ianze, diamond platnumz aliongea kwa utani akidai kuwa yeye ndiye msanii wa kipekee ambaye ameingia kwa tamasha bila mpenzi kwani bado hajapata mpenzi baada ya kuachana na tanasha Donna.

jihan Dimack miss universe Tanzania

” Kama mnavyojua, tamasha kama hili tunatakiwa kuwa na wapenzi wetu ubavuni lakini kama mnavyoelewa Mimi ndio pekee kutoka wasafi mwenye hana mpenzi.. naomba mnisaidie kuchagua… ” Alisema diamond platnumz.

Wengi walidhania kuwa diamond angeingia kwa tamasha na zari Hassan ambaye kwa mda sasa wamekuwa kwa uhusiano mzuri kama wazazi wawili. Hili halikuwa na ilibidi watu wabidiike watafute Nani mpenzi wa diamond platnumz kwa sasa.

Jihan Dimack

Alipoulizwa kama zari Hassan atakuwa na shabiki mmoja, diamond alisema kuwa chochote chaweza fanyika kwa tamasha maana tamasha yenyewe itakuwa kubwa ila hakusema kama Zari Hassan atakuwa kwenye hiyo sherehe.

Kama kawaida, wengi walihudhuria tamasha Kati yao akiwemo mwanamke aliyewavutia wengi. Mwanamke huyo anafahamika kama Jihan Dimack ambaye alishinda miss universe Tanzania Kati ya mwaka 2016-2017

Jihan Dimack ambaye ana umri wa miaka ishirini na tano alivalia vazi rasmi sawiya na diamond platnumz kwenye tamasha.

Jihan DimackĀ  alipiga picha kadhaa kwenye red carpet. Mama Dangote ambaye ni mamake diamond platnumz aliweka baadhi ya picha zake jihan Dimack. Hapo ndipo mashabiki walianza kumuongelea wengi wakisema huenda akachukua nafasi ya tanasha Donna aliyekuwa mpenzi wa diamond platnumz.

Shabiki mmoja alichangia kwa post ya sanura, mamake diamond huku akisema “.. najua huyu atakuwa shemeji wetu….wenye kufikiria haraka kama Mimi tushajua maana fiche ya hii post… Nasema hivo maana nguo alizovaa ni sawiya na vazi la diamond platnumz…”

Jihan Dimack na diamond platnumz

Mwingine alisema “….kwa wanawake wote walihudhuria tamasha ya leo, umechagua kutuekea picha za jihan Dimack.. tushaelewa huyu atakuwa shemeji yetu”

Jamaa mmoja mwenye anafanya kazi ndani ya wasafi ameunga mkono kuwa Jihan Dimack ni mke mtarajiwa wa diamond platnumz.

“Mimi ni mwanao na nakujua vizuri sana, unapoeka post kama hii lazima iwe na maana yake. Wewe kama mamangu nakuelewa na wewe Sanura Kassim a.k.a mama Dangote ni mwerevu. Wacha tuzidi kungojea mazuri labda August ama September watu watajua ukweli wa mambo…”

Zari Hassan azua gumzo kuhusiana na umri wake halisi

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *