MaishaMchipukoMziki

Picha za mpenzi mpya wa Diamond platnumz

Picha za mpenzi mpya wa Diamond platnumz zinazidi kusambaa kwenye mitandao na kwa kweli diamond ana mpenzi mpya.

Msanii kutoka nchi ya Tanzania Naseeb Abdul juma ambaye wengi wanamjua kama diamond platnumz wiki Jana alieka video kwa Instagram inayomuonyesha mwanamke anayesemekana kuwa mpenzi mpya. Katika hii video wawili hawa walikuwa ndani ya Cadillac Escalade, gari mpya ya diamond platnumz.

diamond platnumz new girlfriend
Diamond platnumz aliwaacha wengi vichwa wazi kwa kumuonyesha mwanamke ambaye wengi walitaka kumjua ni nani.

Kulingana na uchunguzi, mwanamke huyo ashapatikana kwenye mitandao na kwenye Instagram anajiita Cassi scheppel mzaliwa wa Turkish.

Cassi ni mwanamke mrembo na anaonekana class yake ni ya hali ya juu na sasa ameingia kwenye group ya wanawake ambao diamond platnumz ashakuwa nao. wenzake wenye washakuwa na diamond platnumz ni wema sepetu, hamisa mobetto, tanasha na zari Hassan.

Juma Lokole ambaye ni mmoja katika familia ya Diamond platnumz amesema kwamba mwanamke huyo ni mpenzi mpya wa Diamond platnumz na wamekuwa pamoja kwa miezi sita.

Cassi scheppel Diamond platnumz girlfriend

Diamond platnumz juzi amenunua gari mpya hivi majuzi aina ya Cadillac Escalade iliyogharimu zaidi ya dollar laki tatu. Gari hili litakuwa la pili maana ana gari kama hilohilo alilonunua hapo awali.

Katika hii video Diamond alijirekodi akiimba nyimbo mpya “christened loyal” ambayo bado haijaachiwa. Cassi scheppel alionekana akifurahia maneno ya nyimbo hiyo na inaonekana anaijua zaidi. Nyimbo yenyewe inaonekana ikiachiwa itakuwa hit song.

Kuna wakati Diamond platnumz alisemekana kuwa anatoka na Andrea Abrahams baada ya wawili hawa kuonekana kwa live Instagram na wawili hawa walionekana wakiwa na furaha.

Picha za mpenzi mpya wa Diamond platnumz

Kwa sasa bado haijakuwa wazi kama mwanamke huyu atakuwa mpenzi mpya wa Diamond Ila bado twangojea matokeo. Kumbuka Diamond platnumz aliwahi kuwa na tanasha kutoka Kenya ila uhusiano wao haukuendelea japo wawili hawa walizaa mtoto mmoja pamoja kwa jina Naseeb junior.

Sio tanasha peke yake, diamond aliwahi kuwa na uhusiano na hamisa mobetto ambaye alichangia diamond platnumz kuachana na zari Hassan kutoka nchini Uganda.

Wakati huo, diamond platnumz alizaa na hamisa mobetto mtoto mmoja kwa jina Dylan naye Zari Hassan akamzalia mvulana na msichana.

Kama Kuna msanii anayeongelewa sana ni diamond platnumz, sio kwa mziki tu Ila pia kwa vituko vyake na familia yake nzima. Ni mwanamziki wa kipekee afrika mashariki ambaye amepata mafanikio zaidi kuliko wasanii wengine

Kwa sasa Diamond platnumz ni msanii wa kipekee ambaye amekuwa na uhusiano wa wanawake katika nchi tatu za afrika mashariki zikiwemo Kenya, Uganda na tanzania.

Kulingana na Diamond platnumz yeye anataka azae watoto zaidi ya sita. aliyasema hayo alipokuwa anahojiwa na wasafi FM Radio.

Kamata – diamond Platnumz

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *