Maisha

Nyumba ya Akothee inayofanana na ikulu | Tazama picha

Akothee ni msanii wa kike aliyezaliwa nchini Kenya. Ni msanii anayejituma sana kwa kazi ya mziki na huwa tayari kulipa mamilioni ya pesa ili kufanikisha safari yake ya Mziki. Kwa sasa amefanya colabo na wasanii wakubwa barani africa akiwemo Diamond platnumz kutoka nchi ya Tanzania, Mc Galaxy na Mr Flava kutoka nchini Nigeria.

Akothee ni msanii anayependa kutetea haki za wamama sanasana walioachwa na waume zao na kuachiwa jukumu ya kuwalea watoto wao bila kutegemea bwana zao. Akothee ni mmoja wao kwani aliachwa na baba wa watoto wake huku akiachiwa watoto zaidi ya watatu kuwalea.

Bidii yake imemfikisha sehemu hakuwahi kufikiria kama itakuja siku maisha yake yawe ya kifahari.  Akothee ni mwanamziki anayesemekana kuwa na hela nyingi afrika mashariki na kama sio wa kwanza basi huenda akawa kati ya wale wasanii tano wenye hela ndefu.

Kwa sasa msanii huu wa kike ameweka historia baada ya kujenga nyumba moja kubwa sana. Nyumba yenyewe iko migori na inasemekana kuwa kiwango chake cha pesa ni zaidi ya milioni themanini.

Tazama picha zaidi za Nyumba ya Akothee

Watoto wa Akothee Akothee na watoto wake Compound ya Nyumba ya Akothee

Soma hii pia ( Niko tayari Kuolewa :  Betty Kyalo)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *