Mchipuko

Rais Uhuru Kenyatta ameelezea vile uchumi wa kenya utakavyo fufuliwa

Rais Uhuru Kenyatta ameelezea njia nane zitakazotumika katika harakati ya kufufua na kuinua uchumi wa kenya.

Amesema zaidi ya bilioni hamsini na tatu zitatumika kujenga upya zile nyumba na sehemu zenye zimeharibiwa na mafuriko katika sehemu mbalimbali nchini. Pia pesa hizo zitatumika kuongeza walimu zaidi na kusaidia biashara ndogondogo.

Rais Uhuru Kenyatta alisema lazima njia itafutwe ya kujenga upya uchumi wa Kenya na mpaka tatizo la virusi vya corona litatuliwe ili kupatikane mbinu za kuishi na virusi vya Coronavirus. Haya yote alisema jumamosi ya leo mida ya asubuhi.

Bilioni tano zimetemgwa ili kurekebisha barabara zilizoharibiwa na mafuriko na hata daraja na njia zinazotumika na wakenya.

Rais Uhuru Kenyatta pia ametenga bilioni sita unusu katika wizara ya elimu na kutangaza kuongeza walimu elfu kumi na interns elfu moja wa secta ya mawasiliano. Hawa interns watasaidia upande wa masomo kidigitali. Elfu Mia mbili hamsini pia zimetengwa kuboresha madawati.

Bilioni 1.7 zitatumika kuongeza vitanda ndani ya hospitali za uma na pia kwa kuwaongeza wafanyi kazi wa afya elfu tano waliohitimu.

Hii ni baadhi tu ya secta alizoekeza Ila zipo zingine ambazo sijazitaja. kwa mengi zaidi tazama hapa kwa niamba ya citizen Tv. Familia zenye hazina uwezo wa kupata chakula pia hawakusahaulika kwani zaidi ya milioni 250 zitatumika kuwalisha kila wiki.

Rais Uhuru Kenyatta akihutubia wananchi

Kulingana na Rais Uhuru Kenyatta, huenda wakenya wakarudi kwa Hali yao ya kawaida na kwa Sasa wanatafuta njia mwafaka yenye itatumika ili kujikinga na Coronavirus. Hii itasaidia kujenga Kenya kwani kwa Sasa uchumi umeenda chini

Soma hii pia ( vyakula vinavyoongeza damu mwilini)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *