Sanaa

Sauti Sol waangukia dili ya mamilioni ndani ya Netflix.

Wasanii tajika sauti Sol wanazidi kunufaika na bidii yao baada ya kupata dili mpya na Netflix. Kama unakumbuka vizuri, sauti Sol ndio waliweza kulipwa hela nyingi na MCSK isiopungua laki nne.

Siku kadhaa baada ya kuachia nyimbo yao mpya Suzanna, mambo yao yanazidi kunyooka zaidi na huenda wakalipwa mamilioni ya pesa baada ya kuhusika kwa series mpya kutoka afrika kusini inayojulikana Kama “queen sono”

Series ya queen sono ilianza kuonesha Jana ndani ya nexflix original. Sauti Sol wametangaza kuwa wataachia album mpya hivi karibuni. Album hiyo itakuwa na nyimbo za ushirikiano wa wasanii kutokea nchi mbalimbali akiwemo burna Boy, Sho Madjozi na India Arie.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *