Serikali ya Kenya yatangaza uwepo wa Corona virus nchini
Waziri wa afya ametangaza rasmi kuwa wamepata kesi ya kwanza nchini ya virusi hatari vya Corona virus. Mwanafunzi mmoja mkenya amepatikana na Corona virus Leo asubuhi. Inasemekana mwanafunzi huyo aliingia Kenya kutoka amerika.
Katibu mkuu wa wizara ya afya mutahi kagwe amesema waweza kufuatilia wale wote aliweza kuwasiliana ama kuwa na ukaribu nao kwa huu mda mfupi amekuwa nchini Kenya. Inasemekana kwa Sasa hali yake ya kiafya imeimarika Ila anaendelea na matibabu katika hospitali ya Kenyatta.
Mutahi kagwe ametoa tahadhari na kutaka wakenya wazingatie sana usalama wao wa kiafya akiwahimiza wakenya waweze kunawa mikono yao kila Mara, huku akiongezea kusikuwe na mikutono ya hadhara.