MaishaMchipuko

Stivo simple boy apata dili ya hela ndefu

Walisema wahenga zama zile kwamba, bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi. Kwa sasa Stivo simple boy ni mwingi wa furaha na sasa hivi anafurahia matunda ya bidii yake.

Alipoanza mziki, wengi walimtupia maneno na matusi chungu nzima. Wengi hata kumkejeli na kusema ana sura mbaya. Kwa kweli Mungu amewakosoa wote wale walidhania stivo simple boy haendi popote.

Stivo simple amepata dili na kwa sasa ni balozi wa odi bet. Kutokana na cheo chake kipya katika odi bet, msanii huyu amefanya tangazo la kwanza na kampuni hii ya betting na inasemekana amelipwa mamilioni ya pesa.

Tangazo hilo la odi bet amelifanyia haki na wakenya wamempongeza kwani hawakutegemea kama ana uwezo wa mkubwa hivi wa kuigiza.

Kumbuka stivo simple boy aliwahi kupata tuzo la msanii bora wa kiume nchini kenya baada ya kupata Kura nyingi kutoka kwa mashabiki wake. Hii Ina maana wakenya wengi wanapenda bidii yake na wanampa sapoti inayostahili.

Pongezi sana simple boy kwa cheo chako kipya na hapa mwangaza news tunakuombea mola azidi kubariki kazi ya mikono yako.

Soma hii pia: Mpenzi Stivo simple boy

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *