International

Tajiri mashuhuri kutoka Nairobi kwa jina joe Kariuki avamia mji wa mombasa

Baada ya kutatiza jiji la Nairobi, mfanyi biashara mashuhuri anasemekana kuhamia mji wa mombasa. Baada ya kukaa Nairobi na kufanya biashara zinzosemekana kuwa na utata, mfanyi biashara huyu ameamua kukita kambi mji wa mombasa ili kuendelea na biashara zake Kanda ya pwani.

Kulingana na uchunguzi wa kina, joe Kariuki ambaye ndiye mwenye kampuni ya cryptocurrency company 51 capital amefungua kituo kingine sehemu inayojulikana kama bamburi ilioko mombasa. Biashara hii yake mpya inaonekana kuvutia wanawake kwani wengi wameonekana wakifurika ofisini humo ili kuweza kufanya Kazi kwa kampuni hiyo. Katika picha zilizotufikia wanawake wanaonekana ndani ya ofisi na pia wazungu huonekana pia kwa hiyo ofisi.

Joe Kariuki ni mfanyi biashara ambaye huewezi kuelewa shughuli zake kwani ni juzi alisemekana kuendesha muungano wa “powered up iliozua maswali kwani ilisemekana anawasajiri matajiri ikiwa Nia yake haileweki ni nini. Kulingana na ripoti za hapa na pale, ilisemekana watu hawa wangekuwa matajiri zaidi wakiendelea kufanya Kazi naye

Wanawake Wenye wanafanya Kazi kwa kampuni ya joe Kariuki wanasema wanachokifanya ni sawa na hakuna kibaya kinachoendelea.

“Mimi nimemjulia Joe Kariuki kwa mtandao. Nimemjulia online. Nimemskia na vituko zake na wakati ilipotangazwa kuwa anafungua ofisi Mombasa nikawa interested kutembea na kujua kile anachokifanya huku. Ndipo nikam-meet na kugundua kuwa ni mtu mzuri tu mwekezaji lakini watu wengi wana taswishi naye. Ila mimi sina shida naye kwa sababu nimeona uwezo wake na yale mambo ambayo anafanya yanasaidia vijana sana. Sisi warembo wa Pwani tumechoka kutumiwa vibaya ndiposa tuko nyuma ya Joe Kariuki kwa sababu inaonekana anatujali na pia tunapata pesa ipasavyo, “ Aisha Mohammed* (not her real name) said to us.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *