MaishaMchipuko

Tamthilia ya Pete yampoteza muigizaji mwingine

Pete ni tamthilia inayopeperushwa ndani ya maisha magic na maisha magic plus ndani ya DSTV. Ni tamthilia inayopendwa na wengi na imekuwa ikiperushwa zaidi ya miaka mitatu kwa sasa.

Mwaka uliopita, tamthilia ya Pete ilimpoteza Gillie Owino aliyekuwa akijulikana kwa jina la “Mzee msiri. Ilibidi atafutwe muigizaji mwingine ili kuziba pengo lililoachwa na Mzee msiri.

Leo asubuhi tarehe 5 mwezi wa pili mwaka wa 2022, Pete imempoteza muigizaji mwingine aliyekuwa akijulikana kama mermaid hunter ama mwidaji chunusi.

Telly Savallas mwidaji chunusi
Telly Savallas : Mwidaji chunusi

Ni siku ya huzuni kwa wapenzi wa tamthilia ya Pete kote afrika mashariki kwani kufikia sasa Pete maisha magic wamewapoteza wasanii wawili tangu ilipoanza kupeperushwa.

Poleni sana kwa waliofiwa, mwenyezi mungu awape nguvu wakati huu mgumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *