MaishaMchipuko

Tanasha Donna :Nimekuwa nikikufikiria, Kunani?

Tanasha Donna amerudi tena kwenye mziki na wakati huu anaonekana akiwa na mawazo kwa mtu anayempenda kwa dhati. Tanasha Donna ambaye aliachana na Diamond Platnumz mwezi wa pili mwaka huu anaonekana kama ako karibu kuwa kwenye uhusiano mpya.

Tanasha Donna ambaye jina yake ni Aisha amekili kwamba kunaye mtu anayemfikiria sana na mda mwingine huwa anaota akiwa naye. Hii ina maana mwanadada huyu ataka kuingia tena kwenye mahusiano.

Anasema Roho yake itatulia wakati atakaye mpata wa kumpenda na kuishi naye mpaka siku yake ya mwisho hapa duniani.

Tanasha Donna - Sawa Video

“…I have been loving you, in my dreams, and I’ve been thinking of you endless. Na ka uko hapa niko sawa. I love you forever….”

Akimpata anaye mpenda, atampa roho yake yote na chochote anachokitaka. Atamfanya angare kama nyota. Tanasha Donna ameahidi kujalibu awezalo kuhakikisha chochote kilifanyika kwenye mahusiano yake ya hapo awali hakitarudia tena. Huu ni wakati wa kuponya nyoyo zenye huzuni na sio kwa mpenzi wangu ila kwa kila mtu alioko karibu nami.

Mwanadada huyu ameamua kusahau yaliyopita na kuganga yajao huku akisema yeyote aliyemkosea atamsamehe. Kwa sasa kila mtu anangojea chenye familia ya Diamond platnumz watasema, kama watamsikiza au la. Kumbuka yeye na Diamond Platnumz waliweza kuzaa mtoto mmoja, Naseeb Jnr walipokuwa kwenye uhusiano.

Sawa ndio Nyimbo yake Tanasha Donna, anahimiza watu waweze kupendana, sio kwa wapenzi wao tu ila pia kwa walioko karibu nao. Kwa video ameshirikiana na paskal tokodi na pia Nasseb Jnr ako kwenye hii video.

Soma hii pia { Niliwahi kulia : Mbosso} 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *