Mchipuko

TANESCO huduma kwa wateja ( TANESCO contact)

Kwa wale wamekuwa wakiulizia kuhusu TANESCO huduma kwa wateja, kaa mkao wa kula upate maelezo kamili.

Unaweza ukawasilina na TANESCO kupitia namba ya simu ambayo ni (+255) 768 985 100 ama pia ukatembelea ofisi zao zilioko dar es salaam road plot no. 114 block G ama pia waweza kuwatumia barua P.o Box 453 dodoma. Email address ni communications.manager@tanesco.co.tz

Fahamu mengi kuhusu Tanzania electric supply company ( TANESCO)

TENESCO ni nini? Hili ni shirika la umma lililoko katika wizara ya nishati ( energy). Kazi ya TANESCO ni kuzalisha, kusambaza na kuuza nguvu za umeme ndani ya nchi ya tanzania. TENESCO wanauzia kampuni ya ZECO ilioko Zanzibar ambayo huuza nguvu za umeme kwa visiwa vya ugunja na pemba

Wajerumani ambao walikuwa wakoloni walianzisha usambazaji wa stima mwaka 1908 mjini Dar es salaam. Wakati huo Tanzania ilikuwa inajulikana kama Tanganyika. Ilisaidia sana vituo vya gari Moshi na pia sehemu ambazo wakoloni walikuwa wakiishi.

Mwaka wa 1920, great Britain iliunda kitengo Cha stima ili kusambaza umeme kwa umma hii ni baada ya wajerumani kutoka nchi ya Tanzania.

TANESCO ilianzishwa tarehe 26 November 1931 Ila wakati huo ilikuwa ikijulikana kama Tanganyika electric supply company Ltd. Kampuni nyingine iliyokuweko ni dar es salaam and district electric supply company Ltd ( DARESCO)

TANESCO ilianza Kazi rasmi mwaka wa 1933 na station yao ilikuwa sehemu ya Kange. Mwaka wa 1936 kampuni hiyo ilikuwa na bwawa la maji lenye mita tisini kwa urefu. Bwawa hili lilikuwa karibu na mto wa pangani na lilikuwa na uwezo wa kuzalisha stima kiasi Cha 5MW

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *