TRA huduma kwa wateja na TIN namba
Ningependa kuichukua fursa hii kuongea mengi kuhusu TRA huduma kwa wateja na TIN namba. Najua wengi Wana maswali chungu nzima Ila majibu yote utapata hapa. Tuandamane pamoja mpaka mwisho ili uweze kujifunza mengi.
TRA huduma kwa wateja
Kituo hiki kinaongozwa na Bwana Alphayo J. Kidata ambaye ndiye Kamishna Mkuu.

TRA kwa urefu ni Tanzania revenue authority. Hii kwa kiswahili tunaweza sema ni mamlaka ya mapato Tanzania. Mamlaka hii inatoa huduma nyingi sana kwa wanaichi zikiwemo TRA huduma za mitandao.
Huduma zinazotolewa na TRA ( mamlaka ya mapato Tanzania)
Kati ya huduma za tra ni kama zifuatazo.
- kusajili kama vile biashara yako
- kumshughulikia na Kodi
- Kukaguzi wa Kodi
- Kupeana Kibali cha Forodha
- Kupeana leseni kama za biashara
- Kutatua utata na kujibu maswali yanayohusiana na pesa za umma ama Idaho
- Pia mamlaka hii hutumika kurejesha na kutoa nafuu ya kodi
- Elimu ya Kodi hutolewa na Mamlaka hii pamoja na kuchunguza mambo yanayohusiana na Kodi
- Kutoa data za kitakwimu na kufunza watu
Uingizaji na Uondoshaji wa Bidhaa Nchini
- Viwango vya ushuru
- Viwango-fedha za kigeni
- Taratibu-uingizaji bidhaa
- Mawakala wa forodha Kabla ya mizigo kufika
- Taratibu-utoaji bidhaa
- Leseni za Forodha
- Vyombo vya usafiri
Pia mamlaka ya mapato Tanzania inajihushisha na
- Usajili vyombo vya usafiri
- Kodi ya kubadili umiliki
- Leseni ya mwaka
- Leseni ya udereva
- Kodi na ushuru
- Mapato ya watu binafsi
- Kodi ya makampuni
- Kodi ya Mapato yatokanayo na Ajira
- Uendelezaji ufundi stadi (SDL)
- Kodi ya zuio
- Mapato ya uwekezaji raslimali
- Kodi ya ongezeko la thamani
- Ushuru wa bidhaa
- Ushuru wa stempu
- Michezo ya kubahatisha
Unaweza wasiliana na huduma ya TRA kupitia simu zao ambazo kupiga ni bure.
Nambari zao ni kama ifuatavyo
0800 750 075
0800 780 078
Pia unaweza piga simu kwa namba hii hapa
+255 22-2119343
Barua Pepe:huduma@tra.go.tz
Facebook: tratanzania
Twitter: tratanzania
Instagram: tratazania
TRA TIN namba
Kuna maswali mengi huulizwa kuhusiana na TIN namba na jinsi ya kupata TIN namba online.
Kupata TIN namba online ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kuingia tovuti ya www.tra.go.tz alafu Kuna sehemu imeandikwa usajili wa TIN, bonyeza hapo. Utatakiwa kuweka namba yako ya Nida na ya simu alafu fuata maelezo yanayofuata kwa kujaza form hiyo ili uweze kusaji TIN namba yako.
Kumbuka ukisapata TIN namba online, utakuwa uko tayari kutumia huduma hii na mda mwingine utakapotembelea tovuti hii, basi Kazi yako itakuwa rahisi kwani utaenda moja kwa moja kwa TRA TIN Login na baada ya kuingia utapata huduma ya TRA. Ndani ya tovuti ya TRA, unaweza ukapata lesini ya biashara online ama Kurenew leseni ya biashara. Kuna mtu aliniukila ” Nataka kujua TIN namba yangu” kama umesajili itabidi uingie ndani ya tovuti ya TRA, weka number yako ya Nida na ufuate maagizo.
Kama utakuwa hauna namba yako ya Nida au NIN, unaweza pata TIN namba. Unachotakiwa kukifanya ni kufika katika kituo Cha TRA na kadi yako ya Kura au barua ya serikali ya mtaa, utachukuliwa alama za vidole na utaweza kupata TIN namba.
Kumbuka kupata TIN namba haulipishwi na unaipata bure.
Yafuatazo na majibu ya baadhi ya maswali kuhusu TIN namba
TIN namba ni namba inayotumika kutambulisha mlipa Kodi. Namba hii inaweza tumika Mara mbili aidha kwa mfanyi biashara ama mtu mwenye hafanyi biashara. Unaweza tumia TIN namba kwa malipo ya kodi katika biashara yako ama ajira na vilevile inaweza tumika kulipia ada ya leseni ya udereva.
Kama una biashara ama unapata ajira, unatakiwa kuwa na TIN namba ili uweze kulipa Kodi. Hii ni Sheria iliyowekwa katika kitengo Cha usimamizi wa Kodi. Kama unapata ajira, haimanishi utachukua TIN namba nyengine. Hiyohiyo ndio itakayotumika kwa shughuli zote mbili.
Kama una leseni ya udereva na ungepata kujua TIN namba yako unachotakiwa kufanya ni kufika kituo Cha TRA na utapata TIN namba yako.
Kwa Leo tutakomea hapo kuhusiana na TRA huduma kwa wateja na TIN namba. Kumbuka hapa mwangaza news tunakuelimisha na pia tunakupa matukio mbalimbali kutoka pande zote hapa duniani.