Mchipuko

Ugomvi wa Wolper na Aunt Ezekiel

Kama umekuwa ukifuatilia story za bongo movie basi utakuwa umekutana na nyingi stori kuhusiana na Ugomvi wa Wolper na Aunt Ezekiel. Kwa mda sasa wamekuwa wakirushiana majembe ndani ya mitandao na kwa kweli wawili hawa hawana maelewano mazuri kwa sasa. Sio hivyo tu, kama ulikuwa hujui, Ruby huwa hawaelewani na Aunt Ezekiel baada ya Kusah kutoka kwa Ruby na kuanza mahusiano mapya na Aunt Ezekiel.

Picha za harusi ya Wolper na Rich Mitindo
Jackeline Wolper Na Rich Mitindo

Kulingana na ripoti sa hapa na pale, Irene Wolper na Aunt Ezekiel walokosana kabla ya harusi yake Wolper na Rich Mitindo. Inasemekana aunt Ezekiel ndiye alikuwa mwenyekiti wa kamati ya kupanga harusi ila Cha ajabu hakutokea kwenye harusi ya Wolper. Ugomvi wao ulianza wakati wa kupanga harusi kwani Aunt Ezekiel alisemkana kutokuwa makini na mipangilio ya harusi na alikuwa akiitana mikutano kwa mda anaotaka

Habari za hapa na hapa zinasema kwamba, aunt Ezekiel amekuwa mkaribu wa ex yake baba T ambaye kwa sasa ni mme wa Wolper. Inasemekana ni kama yuamfanyia kampeni ya kurudiana na baba T. Aunt Ezekiel ana historia sana kwani ashawahi kuwa kwenye uhusiano na Mose Iyobo na wako na mtoto pamoja

Aunt Ezekiel na Mose Iyobo
Aunt Ezekiel na Mose Iyobo

Aunt Ezekiel na Wolper wamekuwa waki post kwa mitandao kila mmoja akioneka kumuongelea mwenzake. Kuna wakati Aunt Ezekiel Ali post mambo ya kutumia vigodoro na ni kama hii post ilikuwa yaelekezwa kwa Wolper kwani Ezekiel mwenyewe ana shepu na huenda anaamini kuwa Wolper anatamua vigodoro.

Ruby na kusah
Ruby na kusah

Wolper naye alionekana kumpa tahadhari Ruby na mpenzi wake mpya na kumuhimiza amchunge sana mpenzi wake asije akachukuliwa na atakuwa anamanisha kuchukuliwa na aunt Ezekiel kwani Kusah ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Ezekiel, alikuwa mpenzi wa Ruby kabla ya kuanza mahusiano na Aunt Ezekiel.

Kusah Aunt Ezekiel
Kusah Aunt Ezekiel

Aunt Ezekiel na mpenzi wake Kusah walifikia hatua mpaka ya ku unfollow Irene Wolper na chakushangaza ni kwamba bado Wana follow baba T ambaye ni mumewe Wolper. Watu wameshangazwa na hatua ya Kusah kwa kuingilia mambo ya Wolper na Aunt Ezekiel na kufananisha hatua ya Kusah kama ya kike. Kusah angekuwa muungwana kama baba T na kuacha hawa wawili washuluhishe mambo Yao

Tutazidi kukupa mengi kuhusianana Na Ugomvi wa Wolper na Aunt Ezekiel kwa hivyo zidi kutegea hapa mwangaza news kwa mengi zaidi

Soma pia Historia ya Mandonga

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *