MaishaAfya

Ugumba ni nini : Ugumba kwa wanaume

Leo katika kitengo Chetu Cha afya nataka tuongelee tatizo la ugumba kwa wanaume. Hili ni tatizo linalowatatiza sana wanaume na wengi hawajui kama ugumba unatibika.

(Ugumba in English ) sterility ama barrenness ndio majina yanayotumika na wazungu.

Kwa wale wote wamekuwa wakiulizana ugumba ni nini, nataka kuwalezea. Ugumba ni hali ya mwanamke au mwanaume kushindwa kutekeleza tendo la ndoa. Hii inaweza ikaathiri hata kutozalisha ama kuzaa kama wewe ni mwanamke.

Watu wengi sanasana waume hugopa kusema wanapojipata na tatizo kama hilo kwani wao huona ni aibu kusema mbele za watu. Wengi huenda hata wakaachwa na wapenzi wao kwa kushindwa kutimiza majukumu ya kizazi.

suluhu la tatizo la ugumba

Cha ajabu ni kwamba wanaume huwalaumu wanawake wao na kudai kwamba wao ndio wenye tatizo ili kujiondolea lawama. Ukweli ni kwamba hili tatizo huwa upande wao.

Katika utafiti wa madaktari waliohitimu duniani, wanaume asilimia kumi na tano Kati ya wanaume wenye umri Kati ya miaka 18 mpaka 35, Wana tatizo la ugumba.

Utafiti zaidi unaonyesha kwamba wale wanaume waliofikisha miaka 40, zaidi ya asilimia 40 wameathirika na ugumba. Hawa wanaume wanapitia wakati mgumu kwani ni vigumu kwao kuwatosheleza wanawake wao sabubu ikiwa tatizo kwenye nyeti zao.

Wanaume kama hao hujitenga sana kwani huogopa kusemwa na majirani na hata jamii yao. Wengi hutorokwa na wapenzi wao ambao huenda kutafuta wanaume wengine wanaoweza kuwatimizia mahitaji yao ya ndoa.

Aina za ugumba

Mwanamke huyu ama mwanaume ambaye ana shida ya ugumba huogopa tu ile siku Siri yake itajulikana. Wakati huo itabidi ahame mji ama labda ajifungie kwa nyumba kwa kuogopa kusemwa. Kumbuka wanaozitoa Siri hizi ni watu wa karibu na anayehusika.

Wanaume wenye wameathirika huogopa hata kujihushisha na mazungumuzo yanayohusiana na ugumba kwani huona kama wanaongelewa wao.

Ukiwa na hali hii, magonjwa mengine hujitokeza na pia usisahau mawazo yatakusumbua na ikifikia hapo utaogopa hata kujaribu kushiriki tendo la ndoa kwani wajua wazi kuwa hautofaulu.

Basi hapo ndipo mke wako atakuwa mkali nyumbani na hata huenda akasema umeshindwa kushiriki tendo la ndoa maana uko na mwanamke mwingine kumbe maskini una tatizo katika sehemu zako za Siri. Ugomvi bila sababu yoyote utazidi kutokea na kila siku itakuwa ni vurugu tu.

Kunaye daktari mmoja kutoka nchi ya marekani kwa jina Rasheed Adedapo Abassi. Daktari huyu alisomea chuo kikuu Cha Yale. Hujihushisha sana na afya ya wanaume na amefanya Kazi hii kwa miaka 19.

Kulingana na yeye, ana majibu mengi kuhusu ni kwa nini mwanamke anakosa kupata ujauzito, ni njia gani anaweza kujitibu na vipi anaweza kujizuia na hali kama hii.

Hajakomea hapo kwani pia anaelezea sababu zinazomfanya mwanamume kulemewa kushiriki tendo la ndoa na mpenzi wake.

Kama wewe ni mwanamume na huwezi kushiriki tendo la ndoa kwa mda wa dakika 15 basi utakuwa na tatizo katika sehemu zako nyeti. Sehemu hizi hushindwa kuwa tayari, kwa kizungu wanasema Erectile dysfunction kwa kifupi ( ED).

Ili kufahamu kwamba una uwezo wa kushiriki tendo la ndoa, lazima sehemu zako za Siri kama mwanamume ziwe na mihemko unapoamka asubuhi. Kama alfajiri unapoamka haupati mihemko katika sehemu zako za Siri, basi utakuwa na tatizo la ugumba. Hii inamanisha utakuwa huwezi kushiriki tendo la ndoa.

Ugumba husababishwa na nini

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazosemekana kuichangia hali hii. Kumbuka sababu zenyewe zipo nyingi Ila tutapitia kadhaa.

1. Uchache wa homoni za kiume mwilini ama kukosa kabisa.

Mwanamke ama mwanamume, wote wako na homoni japo zipo tofauti. Homoni za mwanamke zaitwa estrogen kwa kizungu huku za mwanamume zikipewa jina la testosterone. Testosterone ndizo zinawafanya wanaume wajihisi waume nazo estrogen ndizo zinazomfanya mwanamke apate uja uzito.

Pia kwa mwanamke, umri huchangia kupungua kwa hormones za estrogen katika miili ya wanawake. Hii sanasana hutokea mwanamke anapofikisha miaka hamsini.

Tukija kwa wanaume kesi yao ni tofauti kwani badala ya homoni kupungua, wao hukabiliwa na changamoto nyingi na zingine zinaweza rekebishika kama hazitapuzilia.

Msongo wa mawazo au depression.

Tatizo la shinikizo la kiakili hupatikana sana kwa wanaume. Hii ndio Sababu kuu inayosababisha ugumba miongoni mwa wanaume wengi. Hali hii ya msongo wa mawazo huletwa na mambo kadhaa kwenye maisha ya wanaume kama vile kutokuwa na Kazi, ukosefu wa pesa ama pia changamoto katika familia ama kwenye ndoa.

Kutofanya mazoezi

Mazoezi husaidia kuondoa tatizo kama hili. Unapofanya zoezi, Moyo hupata uwezo mkubwa wa kusukuma damu na kuiwezesha damu kuzunguka kwenye misuli yote mhimu. Hii itakuepusha na tatizo la Sonona linaloletwa na damu kuganda mwilini. Kulingana na daktari Abbas, pia kufanya tendo la ndoa Mara kwa Mara ni mazoezi.

Dkt Abbas anawashauri wenye ndoa kushiriki tendo la ndoa Mara 21 kila mwezi hii Ina maana una siku saba tu za kutofanya tendo la ndoa kila mwezi. Bali na kumaliza shida ya ugumba, Utafiti unaonyesha wazi kwamba, kushiriki katika tendo la ndoa Mara kwa Mara kunasaidia kuepukana na saratani ya tezi dume

Kukosa ama kutotumia maji Safi.

Wengi huenda wakaona hili suala haliwezi kuwa lachangia  tatizo la ugumba Ila ukweli ni kwamba linaweza na hii ni Kulingana na daktari Abbas. Kama maji itakuwa haina virutubisho mhimu, basi huenda ikachangia kuzorota kwa afya ya uzazi haswa kwa wanaume.

Kumbuka sio tu kwa afya ya uzazi Ila maji machafu huathiri afya kwa jumla. Daktari Abbas anawahimiza watu wote kunywa maji Safi na ikiwezekana waweke dawa ya Fluoride calcium ama selenite.

Kumbuka kwamba ugumba unatibika. Unachotakiwa kukifanya ni kumshughulikia tatizo lolote utakaloliona kwa sehemu zako za Siri haraka iwezekanavyo na usingojee mpaka wakati tatizo limekuwa kubwa.

Kulingana na utafiti wetu, ugumba na utasa una tofauti kidogo kwani kunao tasa wako vizuri kwa kufanya tendo la ndoa japo mayai yao hayana nguvu za kuleta mazao ila kama una ugumba, sehemu zako za Siri huenda zikakataa hata kusimama.

Kwa Leo tutakomea hapo kuhusiana na tazito la ugumba kwa wanaume. Asanteni sana kwa kuzidi kuzifuatilia taarifa zetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *