Maisha

Uhusiano wa mama Dangote na princess Tiffah

Mama Dangote na princess Tiffah wanaonekana kuwa na uhusiano mzuri sana. Japo diamond platnumz ana watoto kadhaa nje ya ndoa, inaonekana ana chaguo lake la anayependa zaidi

mama Dangote, zari hassan diamond platnumz

Princess Tiffah ambaye ni mwanawe Diamond Platnumz ni kweli yuapendwa na nyanyake. Inaonekana amemuweka pahali pema kwa roho yake.  Kwa Mara nyingi, mamake diamond platnumz hueka post za princess Tiffah na hii inaonyesha mapenzi ya wawili hawa.

Kama umekuwa ukifuatilia mitandao na ukapata bahati ya kukutana na video ya mtoto huyu, utakubaliana na Mimi kuwa kila hatua anayoipiga ni kana kwamba anafuata nyayo za mamake.

mama Dangote, princess Tiffah

Mama Dangote ambaye ni nyanyake Tiffah humjaza kwa mitandao bila hata kufikiria marambili ikizingatiwa kuwa diamond platnumz ambaye ni mwanawe hawako kwa uhusiano na Zari Hassan ambaye ni mamake Tiffah. Maneno anayoyaandika akimzungumzia Tiffah huwa matamu na ndio maana tukasema mama Dangote anampenda princess Tiffah.

Je wajua Princess Tiffah ni mpishi, kama ulikuwa hujui basi lifahamu hili. Ninaposema mtoto huyu anajua kupika simanishi chakula ya kawaida kwani mtoto huyu hupika hata chapati. Tazama video yake akipika

Video inayofutia ni ya princess Tiffah akimtakia bibiye mama Dangote siku njema ya kuzaliwa. Maneno yake yanaonkena matamu, tazama hapa

Kuna video nyingine ya princess Tiffah akiongelea utajiri wa babake. Kwenye video hii anaonyesha vile babake ana hela nyingi na ni kweli mtoto huyu anaelewa bidii ya babake. Pia anasifia mapenzi yake na babake.

Mwaka wa 2019 mwezi wa nane wakati wa kusherehekea siku ya kuzaliwa ya princess Tiffah, mama Dangote alionekana ku post video nyingi akimsifia Princess Tiffah. Wakati huo princess Tiffah alikuwa mdogo na alikuwa anaanza kuota meno

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *