Mchipuko

Uhusiano wa Marioo Na Paula ni wa kweli ama ni kiki?

Pichani ni wapendanao Paula Kajala na Mwanamuziki Staa wa Bongofleva Omari Mwanga maarufu kama Marioo wakiwa kwenye pozi la kimahaba linalodhihilisha kwamba wawili hao wamezama haswaa katika penzi lao.

Akiwa nusu utupu, tumbo, kitovu na viungo vingine ninavyotakiwa kustiriwa vikiwa nje, Siku ya jana Paula alipanda jukwaani na kuanza kucheza kwa kumnengulia mpenzi wake Marioo wakati alipokuwa akitumbuiza jukwaani, ambapo mbele ya macho ya mama yake Kajala Masanja, Marioo na Paula walipigana mabusu ya hasara hasara bila kujali camera za Wanahabari zilizokuwa zimewazunguka.

Kitendo hicho kimewaibuwa Watanzania, wengi wao wakiwa ni watu wazima ambao wameonyesha kusikitishwa na mfumo wa maisha aliouchagua Paula kuanzia mwanzo alipoanza kujulikana hadi sasa, wanasema maisha ya kujianika na kutoka kimahusiano na kila mwanaume, kwa sasa yatampa umaarufu na pesa lakini yanamuharibia maisha yake ya baadae atakapohitaji kutulia na kuwa mwandani wa mtu fulani.

Walimwengu hao wanasema hata haya mahusiano hayatafika mbali wataachana na atakuja mtu mwingine atajipachika kwa muda mfupi kisha ataondoka na idadi itakuwa inaongezeka ( Baadhi ya Wanamuziki wa kiume wakiwa chemba wamesikika wakisema ni mwendo wakupokezana kijiti, ni kama folen, kila mtu anatamani apite ile sehemu kwa gharama yoyote ile kisha akifanikisha anapisha anaingia mwingine).

Kwa alivyoanza kujulikana Paula, kutokana na shule akiyosoma alitakiwa sasa hivi awe Chuo akipambana na masomo kama ilivyo kwa wenzake wakina Sonia Monalisa, la hasha!!! kama shule ni shida kwake basi angalau angefanya mambo yake kimyakimya na siyo kupanda jukwaani na kuanza kunengua mauno akiwa nusu utupu, hata Wema na Kajala walikuwa hivyo hivyo lakini matokeo yake kila mtu anayaona.Wamesema Walimwengu.

Kwa upande wako unamtazamo gani juu ya hili we SEMA tu UKWELI kwenye comment?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *