Afya

Watu wahimizwa kuvaa Barakoa ( Mask) wakati wanafanya tendo la ndoa

Tendo la ndoa lazidi kuwa ngumu;…Walioko kwenye uhusiano wa kimapenzi wamepata pigo kubwa kwani wamehimizwa kutumia barakoa wakati wanapofanya tendo la Ndoa. Hii ni kuzuia kuambukizana virusi hatari vya corona hii iliweza kusemekana na wataalamu wa Havard university researchers na habari hii iliweza kuandaliwa na mtandao wa Toronto sun

Ugonjwa wa Corona unazidi kubadilisha maisha ya watu wengi na kwa sasa ni kama kila mtu anapitia maisha ya wanaopitia wafungwa huko magerezani. Barakoa zimekuwa ndio mtindo wa kila siku na kila unayekutana naye basi atakuwa amevalia. Nchi nyingi ziweka sheria na ukipatikana haujavalia kifaa hichi basi huenda ukashtakiwa au hata kulipa hela nyingi.

Wakati huu nchi nyingi zimefungwa kwa wastani na wapenzi wengi wanatumia mda wao mwingi kubakia majumbani mwao. Hivyo basi wanaoshiriki tendo la ndoa wametahathalishwa waweze kutumia njia za kujikinga na ugonjwa huu.

tendo la ndoa

Wametakiwa ikiwezekana wawe wanavaa barakoa wakati wote wanapofanya mapenzi kwani chemichemi za maji zinazotoka ndani ya midomo ama pua husababisha corona kama mmoja ako na virusi vya corona virus. Pia ikiwezekana, wakati wa kufanya tendo la ndoa, wahusika wamehimizwa waweze kusitisha kupigana busu na waweze kuoga mwili mzima kabla na baada ya tendo la ndoa.

Wakati mpenzi wako anapotoka nje na baadaye kurudi nyumbani, huwezi jua amepitia wapi na amekutana na nani. Huenda aliyekutana naye ako na virusi vya corona virus hivyo kuhatarisha maisha yako. Pia watu wamehimizwa kuacha mchipuko na wabakie na mpenzi mmoja kwani hii pia itaweza kupunguza kuambukizana ugonjwa huu hatari.

Soma hii pia ( Habari njema kutoka china)

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *