Mchipuko

Vuta nikuvute kati ya Gavana Joho na Mp wa Nyali Mohamed Ali

Baada ya visa vya Corona kuongezeka county ya Mombasa, serikali ilionelea ni vyema watu waweze kupimwa kwa wingi (Mass Test) ili kubaini ni wangapi walio na virusi kwa manufaa ya wanainchi. Gavana wa county ya Mombasa Ali Hassan Joho alichagua mji wa kale (Old town) waweze kupimwa mwanzo maana huko kuna visa vingi. Cha ajaabu ni kuwa waliojitokeza siku ya kwanza walikuwa kidogo mno na hapo ndipo gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho alipandisha mori na kutangaza lazima watu wapimwe hata kama ni cha lazima la sivyo atawafungia (Lockdown). Mbunge wa Nyali Mohamed Ali alijitokeza kuwatetea wanainchi wa eneo hiyo akisema ni vigumu kulazimisha wanainchi kupimwa ila kinachotatikana ni kuwaeleza kwa upole sababu na manufaa ya kupimwa

Mohammed Ali amesema gavana wa mombasa anafaa kuachia huduma ya afya kufanya maamuzi ila sio yeye. Ali mohamed  amesema katika wakati huu hatufai kutumia nguvu ila wanainchi wanafaa waelezwe kiungwana umuhimu wa kupimwa. Kwa upande wake mbunge wa Nyali amesema anaunga mkono kupimwa kwa watu wote lakini akasema kuwe na utaratibu. Kwa sasa Mbunge wa Nyali amemuomba Gavana joho mwanzo aweze kuwapatia chakula wenye hawana na pia wapewe elimu ya umuhimu wa kupimwa.

Soma hii pia ( Mp wa kilifi aomba msamaha)

tazama video 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *