Sanaa

Waigizaji wa Maria Citizen Tv | Miaka na Majina yao Kamili

Maria ni tamthilia mpya inayopeperushwa kila siku Kati ya saa moja unusu na saa mbili usiku.  Ni kipindi kilichoshika kwa Kasi sana kwani karibu kila sehemu uendapo lazima ukutane na mtu anayeongelea tamthilia hii. Tamthilia hii hupeperushwa citizen Tv na huenda hii imechangia kuwa na watazamaji wengi kwani citizen Tv unaweza kutazama bila malipo.

Kama utakuwa umepitwa na vipindi hivi, Basi jumamosi unaweza tazama Maria Citizen Tv na hapo utaweza kupata episodes zote za Maria  zilizopeperushwa wiki nzima. Kwa wale wapenzi wa mitandao ambao labda hawana mda na runinga, unaweza ukapata Maria kwenye viusasa.

Watarishaji wa Maria Citizen Tv

Maria imetayarishwa na wanahabari wawili ambao ni mke na mme. Wanahabari Hawa wanafanya kazi Citizen. Wawili Hawa ni Lulu Hassan na Rashid abadallah. Ukitaka kuwajua zaidi wawili Hawa Basi jumuika nao kwenye citizen nipashe kila wikendi.

Lulu Hassan pia aliweza kutayarisha tamthilia zinginezo Kama vile Moyo series, Huba ambayo inapeperushwa nchini Tanzania, mchikicho wa pwani na maza iliyokuwa ikipeperushwa ndani ya Maisha Magic.

Maelezo mafupi kuhusu Maria Citizen Tv

Maria ni tamthilia inayoangazia maisha ya Luwi ambaye ni mtoto wa mwisho kwa familia yake. Luwi anampenda Maria ambaye ni mtoto aliyezaliwa kwenye familia maskini. Baada ya kifo Cha mamake, Maria anaenda kuishi na William ambaye ni babake Luwi. Hii inakuwa mwanzo wa Maria kuishi kwenye maisha yenye hakuwahi fikiria. Hata baada ya kuanza kuishi maisha ya kifahari, Maria anaonekana ni yuleyule.

Kabla Maria kuanza kuishi kwa familia ya Luwi, Luwi alikuwa na mapenzi na msichana anayejulikana Kama Sofia. Luwi anaonekana kumpenda Maria punde tu anapoanza kuishi na wao. Jambo hili lamfanya Sofia kukasirika na kuamua kumdanganya Luwi kuwa Ana mimba yake. Luwi anamua kufanya harusi na Sofia lakini bado mapenzi yake yanaonekana kuwa upande wa Maria.

Majina kamili na miaka ya waigizaji wa Maria Citizen Tv

Maria

Maria Citizen Tv

Jina lake kamili ni Yasmin said, ako na miaka 20 na ni Mara yake ya kwanza kuigiza. Utakubaliana na Mimi kuwa Yasmin said amekuwa gwiji katika kuigiza na hakai Kama ni Mara yake ya kwanza. Kusema kweli kuigiza ndani ya tamthilia ya Maria kutamfungulia njia zidi kwani anajua anachokifanya.

Sofia

Bridget Shighadi Sofia Maria Citizen.
Bridget Shighadi | Sofia Maria Citizen.

Katika Maria, Sofia ni mke halali wa Luwi. Anaonekana kuwa na Vita na Maria kwani ni tishio la uhusiano wake. Majina kamili ni Bridget shighadi na ana miaka 27. Ametokea taita na kusema kweli ni mrembo. Kwa wale walikuwa wakidhania kuwa Sofia sio mkenya Basi habari ndio hiyo. Sofia ana mtoto mmoja na Kama unamjua Nick mutuma, Basi ujue ndiye mchumba wake. Wamekuwa kwenye uhusiano na Nick mutuma kwa mda na kwa Sasa uhusiano wao unazidi kunoga. Kama unakumbuka vizuri, Nick mutuma ashawahi kuwa na uhusiano na tanasha.

Mbali na kuigiza, Bridget ni mwana mitindo na pia mwandishi. Ako na fashion design yake inayojulikana Kama ‘yedu’ ianyomanisha yetu kwa lugha ya kitaita.

Luwi

luwi | Maria Citizen TV

Luwi majina yake kamili ni Brian Ogana. Katika tamthilia ya Maria yeye ndiye mume halali wa Sofia japo anampenda Maria. Ana miaka 32 na wanawake wengi huachwa vinywa wazi anapoonekana kwenye runinga. Brian Ogana ameoa na ana watoto wawili. Mbali na kuigiza, Luwi ni mtangazaji /mwanahabari ndani ya goodness broadcasting system (GBS)

Venesa

Venesa Maria Citizen Tv
Venesa Maria | Citizen Tv

Majina yake kamili ni wanjiku Stephens. Anaigiza Kama venessa kutoka kwa familia tajiri. Ni dadake Luwi na Victor. Yeye ndiye huunga mkono Maria hata Kama wengine kwenye familia watampinga. Wanjiku Stephens ana miaka ishirini na tano.

 

Boss William

Boss william Maria Citizen Tv
Boss William

Kwa majina kamili ni dennis musyoka. Yeye ni muigizaji mkuu katika tamthilia hii na anaigiza Kama boss William. Ni babake Luwi na ni ni yeye aliyemleta Maria kwa familia yake baada ya mamake kufa. Yeye ndiye anayetunga na kutoa Sheria katika familia yake.

Vickie aka madam Victoria

Sheila Ndanu Madam Victoria Maria Citizen Tv
Sheila Ndanu | Madam Victoria

Kwa majina kamili Anajulikana Kama Sheila ndanu. Ana igiza Kama mke wa William. Hujaribu sana kuunganisha familia yake. Sheila ndanu ana miaka 55 na pia ni mwanamitindo.

Kobi real

Kobi and Tobi Maria Citizen Tv
Kobi and Tobi

Majina yake kamili ni Linda mukamiwa. Ni mkaribu wa Maria kule kijijini ni pacha mwenzake tobi

Soma hii pia ( Gumzo yazuka kati ya Tamthilia selina na Pete}

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *