MaishaMchipuko

Wanawake warembo Tanzania – wema sepetu hayuko kwa orodha ya warembo

Wanawake warembo Tanzania – wema sepetu hayuko kwa orodha ya warembo ?. Najua unashangaa mwanadada huyu atakosa aje kuwa mmoja wa warembo. Wema sepetu kwa mda sasa amebadilika na kuonekana kama anasumbuliwa na kitu flani. Cha ajabu ni kwamba yeye anasema yupo sawa na alipenda tu kupunguza unene wake.  Mengi yamesemwa kuhusiana na wema sepetu ila sisi tutaachia hapo kwa leo.

Orodha ya wanawake warembo Tanzania

Orodha hii hubadilika kila uchao kwani wengi wanazidi kuzaliwa.hii hapa ndio orodha wa warembo wa Tanzania;

  • Jihan dimack
  • Hamisa Mobetto
  • Elizabeth Micheal “Lulu’
  • Nandy
  • Zuchu
  • Jokate kidoti

Jihan dimack.

jihan Dimack miss universe Tanzania

Ni mwanamtindo mashauri tanzania. Aligonga vyombo vya habari hivi majuzi baada ya kuonekana na diamond platnumz kwenye tamasha ya Zuchu. Wawili Hawa walivaa share na wengi walifikiria labda atakuwa mpenzi mpya wa diamond ila hadi sasa bado hatujaona matokeo. Jihan dimack anatufungulia orodha yetu ya wanawake warembo Tanzania.

Soma hii pia ( je, jihan dimack ni mpenzi wake Diamond)

Hamisa Mobetto

hamisa Mobetto mwanamke mrembo tanzania

Ni mwanamke shupavu na kama kuna mwanamke aliwahi kumkoshesha usingizi Zari Hassan basi ni hamisa Mobetto. Pia yeye ni mwanamtindo ila kwa sasa anajihushisha na biashara tofauti nchini tanzania. Hamisa Mobetto ana mtoto na Diamond Platnumz. Hadi sasa, hamisa Mobetto hana uhusiano mzuri na mamake diamond. Tunapoongelea wanawake warembo, itakuwa sio vizuri tukimkosa hamisa Mobetto kwenye orodha hii.

Elizabeth Micheal ” Lulu”

Elizabeth Micheal - Lulu

Aligonga vichwa vya habari wakati wa kunumba. Ni muigizaji hatari sana na Kama ulikuwa shabiki wa bongo flava basi utakuwa unamfahamu mrembo huu kwa jina elizabeth Micheal. Umaarufu wake ulipata dosari alipohusishwa na kifo Cha marehemu kanumba ila kwa juhudi ya wanafilamu na wanasheria, elizabeth Micheal maaruufu kama Lulu’ aliachiliwa huru. Kwa sasa anashighulika na biashara tofauti.

Nandy mpenzi wake Billnass

Nandy mpenzi wake Billnass

Ni mtoto mwenye muonekano mzuri na swaga za kizungu. Anajua kuvaa na kwake fashion ni Jambo la kawaida. Amekuwa kwa Sanaa ya mziki wa bongo kwa miaka kadhaa kwa sasa na anafanya vizuri sana. Kwa sasa ako kwenye uhusiano na Billnass na wawili Hawa wanapanga kuoana hivi karibuni.

Zuchu

zuchu mwanamke mrembo tanzania

Ni msanii chipukizi ndani ya label ya wasafi. Kwa sasa anawapeleka wasanii wenzake wa kike mbio. Kwa bidii ya wasafi label, zuchu amefikia mbali na kwa sasa anapata wafuasi hata nchi za ulaya. Mziki wake upo kila sehemu na muonekano wake umezidi Kunawili. Zuchu ameingia kwa orodha ya wanawake warembo Tanzania japo hapo mwanzoni alikuwa hajajulikana na wengi.

Jokate kidoti

jokate kidoti kwenye orodha ya warembo

Alikuwa mpenzi wa diamond platnumz na pia mtangazaji. Magufuli alipoingia mamlakani, alimchagua jokate kama mkuu wa wilaya. Alizaliwa 20th March 1987 washington DC. Ashatumika sana kwa video za wasanii na alikiba ashawahi mtumia kwa video zake. Juzi alitangaza kuingia kwenye siasa japo uchaguzi uliopita hakusimama kwa wadhifa wowote.

Wema sepetu

wema sepetu weight loss

Kama kuna mwanamke aliwahi kutesa watu na urembo ni wema sepetu. Aliwahi kuwa miss tanzania. Wema sepetu alikuwa mpenzi wake diamond Platnumz. Kusema kweli warembo wengi tanzania washapitia kwa mikono ya Diamond Platnumz. Wema sepetu alichangia sana Sanaa ya Diamond. Wakati wawili Hawa wanakutana, diamond platnumz alikuwa bado hajulikani kwa hivyo tunaweza sema uwepo wa wema sepetu ulimsaidia Diamond maana hiyo mida wema sepetu alikuwa yuajulikana sana.

Kwa mda sasa wema sepetu amekuwa na mapungufu kwenye mwili wake na afya yake kidogo inaonekana kuzua maswali chungu nzima. Kila akiulizwa yuasema aliamua mwenyewe kupunguza uzani. Hapa mwangaza hatuna habari za kutosha kuhusiana na wema sepetu na kadri tutakapozipata tutawajuza kama ilivyo desturi yetu.

Soma hii pia (Jinsi ya kumteka mwanamke kisaikolojia)

Kuna wanawake wengine labda kwenye akili yako ulidhania watakuwa kwenye orodha ya warembo ila Kulingana na utafiti wetu hawangeweza kujumuishwa. Ili kuwa kwenye hii orodha tumezingatia vitu mingi zikiwemo muonekano wa sura na maumbile ya mwili. Kuna wanawake walikuwa warembo nchini tanzania ila wakapenda chips zege kuliko miili yao na kilichofanyika ni unene tu kwenye miili yao na hivo kuiaga orodha ya warembo Tanzania.

Kwa sasa tutakomea hapo, zidi kufuatilia habari zetu kutoka tovuti yetu ya mwangazanews.

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *