Maisha

Wapwani waraushwa usiku wa manane kisha chai rangi

Ulimwengu haushi vituko na ni Kama Corona virus imeharibu watu akili mpaka wanaamini vitu zenye hazina maana. Usiku wa Jana wapwani wamekuwa wakipokea ujumbe kutoka kwa wenzao kuwa Kuna mtoto amezaliwa na kuwasihi watu wanywe chai rangi bila sukari akidai ni dawa ya Corona. Taarifa hiyo iliongezea kusema mtoto huyo aliaga baada ya kutoa hiyo taarifa.

Bila kufikiria Mara mbili wapwani walichukulia Jambo hilo Kama dharura na asilimia kubwa waliingia kwenye mtego na kupika chai rangi wakidai kuwa wasipofanya hivo wangepoteza maisha yao ifikapo saa kumi na mbili asubuhi.

Jambo hilo limepingwa vikali sana na viongozi wa dini na kuhimiza wanainchi kutoingia kwa mtego Kama huo kwani wanachokifanya ni ushirikina. Kwa wakati huu wa Coronavirus, tunafaa kuwa maskini zaidi kwani habari zingine sio za ukweli. Tusimsahau Mungu na kuanza kuamini

Ningehimiza watu wajaribu kutegemea taarifa kwa vyombo vya habari vinavyoaminika. Kabla ya kuamini maneno ya watu, wafanye uchunguzi wa kina mwanzo.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *