Sanaa

Wasafi Records

Wasafi Records Ni kampuni inayojihushisha na utengenezaji wa mziki. Kampuni hii iko na zaidi ya miaka minane. Diamond Platnumz ndiye mmiliki wa kampuni hii na Kulingana na hapo kampuni imefikia, Basi tunaweza sema kampuni hii imefaulu katika biashara ya mziki.

Wasanii wa Wasafi Records

Kwa mda huu wa miaka nane, wasafi Records wameweza kuwasajili wasanii watano. Wasanii hawa wote wameonekana kufaulu kwani karibia kila msaani aliyesajiliwa WCB anatajika ndani ya Sanaa ya Tanzania na afrika kwa jumla.

Msanii mwenye amesajiliwa hivi maajuzi ndani ya Wasafi Records Ni Zuchu. Zuchu Ni mwanadada anayefanya vizuri sana kwenye sanaa ya mziki. Zuchu Ni dadake Khadija kopa ambaye pia ni mwanamziki gwiji nchini Tanzania. Kulingana na maoni yetu, Zuchu amefanikiwa kwa mda mchache sana na hii inamaanisha mashabiki walikuwa na kiu ya msanii wa kike ndani ya Wasafi Records.

Wasanii wengine ndani ya wasafi Ni Kama vile Mbosso, Rayvanny na Lavalava. Kumbuka harmonize alikuwa mmoja wa WCB Ila aliamua kuanzisha kampuni yake ya mziki kwa jina konde gang.

konde gang harmonize

Msanii Rich mavoko aliwahi kusajiliwa ndani ya Wasafi Records lakini kwa Sasa hayupo Tena. Kulingana na ripoti za hapa na pale, Diamond Platnumz na Rich mavoko walikosa maelewano hivo kukatiza mkataba wao.

wasanii wa Wasafi Records

Kwa Sasa Diamond Platnumz pia anamiliki kampuni ya runinga wasafi Tv ambayo pia imeshika Kasi sana. Hii inaonyesha wazi kwamba, Diamond Platnumz ako na mkono wa biashara na anakielewa anachokifanya.

Diamond Platnumz hushindanishwa na Ali Kiba. Kulingana na mashabiki, Alikiba husemekana kuelewa mziki zaidi kwani mziki wake hudumu kwa mda bila kupoteza ladha. Kwa upande mwingine, diamond platnumz Ni mfanyi biashara na kila anapotumia hela kwa mziki, Basi hutarajia kupata faida.

Diamond Platnumz hupenda sana kufanya shughuli zote na kampuni yake ya Wasafi Records tukianza na audio recording na pia video shooting. Anaye producer wake wa mziki na pia director Kenny ambaye ndiye hufanya video ndani ya wasafi.

Soma hii pia ( uhusiano wa Zuchu na diamond platnumz)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *