MzikiSanaa

Wasanii wa pwani waamua kufanya kazi pamoja.

Mziki wa mombasa wachukua mkondo mpya na huenda muungano wa wanamziki wa pwani ukazaa matunda. Kulingana na kinara wa Sanaa ya pwani John chacha anayejulikana kwa jina la utani Kama “The Don”, wasanii wa pwani wameamua kueka tofauti zao kando na kufanya kazi pamoja.

Wiki mbili zilizopita, wasanii wa pwani na washikadau waliweza kujitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa video ya Ally mahaba akishirikiana na Akeelah. Sherehe hiyo ilifanikiwa huku kila aliyehudhuria akisifu ushirikiano huo.

Juzi pia mfalme wa ziki la Nazi kwa jina maarufu Ally B pia aliweza kufanikisha tamasha ya uzinduzi wa video yake ambapo halaiki ya watu iliweza kujitokeza kumpa sapoti.

Tunawaombea wanamziki wa pwani waendelee na moyo huo huo na bila Shaka watafika mbali.

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *