Mziki

Willy Paul aeleza sababu iliyomfanya aache kufanya mziki wa injili

Msanii tajika Willy Paul anayejulikana kwa jina kamili kama Wilson Abubakar Radido ameeleza wanainchi sababu ya yeye kujitoa kwa mziki wa injili. Akiongea kwenye mahojiano na jalang’o, msanii huyu alidai alikuwa hafurahishwi na wasanii wenzake wa injili.

Kulingana na Willy Paul, wasanii hawa walikuwa wamuonea gere na nia yao ilikuwa aishiwe kimziki ndio maana kila mda walikuwa wakikosoa nyimbo zake za injili. Aliongezea kuwa, yeye kuachana na mziki wa injili haimanishi kuwa hatapata baraka kutoka kwa mwenyezi Mungu maana Mungu huyo mmoja ndiye huwabariki wasanii wa mziki wa secular.

” Mimi na Mungu hatujaachana na nitazidi kuwa mtoto wake, Mungu huyo mmoja ndiye anayewabariki wasanii kama Sauti Sol, Wizkid, David, Burna Boy na pia Chris Brown. Hii Ina maana Mungu hubariki kila binadamu na pia msanii aina yoyote… Sitaki kutaja mtu lakini kabla nitoke kwa mziki wa injili wengi walikuwa hawanipendi.. unakuta mtu ana kuchukia na hujamfanya chochote.

” Kuna watu walishikana na wakagomea mziki wangu huku walihakikisha hauchezwi katika radio na kwa runinga kadhaa huku nchini. Wakati huo nilikuwa nategemea mziki unilishe. Mziki huo huo ndio uliokuwa ukimsaidia mamangu lakini hao watu hawakuwa na huruma na Mimi hata kidogo.. ” alisema will Paul.

Njiwa, nyimbo yake willy Paul akishirikiana na Nandy ndio wimbo wake wa kwanza baada ya kuachana na nyimbo za injili.

” Nafurahi sana kwani saa hii Niko huru kufanya mziki Aina yoyote. Siwekewi mipaka na mtu yeyote. Naweza amka leo nikajiskia nataka kufanya nyimbo ya kumsifu Mungu ama wakati mwingine nijisikie kufanya nyimbo ya mapenzi. Kwa sasa sina mda wa kumbembelezana na binadamu yeyote…”

Alipoingia kwa mziki wa secular, willy Paul alipambana na wengi ambao hawakufurahia uamuzi wake. Wengi walikuwa na chuki zao za kibinafsi ila kwa sasa ana furaha kwani yeye ni Kati ya wasanii nchini Kenya waliofanikiwa kimaisha ambapo kwenye orodha hiyo ako pia Khaligraph Jones.

 

“Wengi Wana chuki na Mimi maana nimefanikiwa katika maisha ya mziki hapa nchini Kenya. Kwa hivyo ninaposema hivo unaelewa chuki inatokea wapi. Nafikiri baada ya Khaligraph Jones, basi hamna mwingine aliyefanikiwa kimziki zaidi ya Mimi na ndio maana namheshimu Khaligraph Jones.

Willy Paul networth

Willy Paul anakumbuka vile alimbembeleza mamake amruhusu aingie kwenye mziki.

“Niligundua kipaji changu nikiwa kidato Cha tatu lakini sikuweza kuokuza talanta hiyo maana mamangu alikuwa hapendi mziki wakati huo. Niliamua kufanya mziki wakati babangu alipoaga dunia. Mamangu bado alikuwa hapendi mziki lakini kwa bahati nzuri kakangu mkubwa alinishika mkono na alikuwa anapenda mziki wangu. Nakumbuka wakati mmoja kakangu alimuongelesha mamangu ili aniruhusu nifanye mziki na kwa bahati nzuri alinikubalia…. Kwa sasa nafurahi kwani mziki naoufanya unasaidia familia yangu iliyokuwa chini kifedha kabla sijaanza mzki…’

Soma hii pia ( video mpya ya willy Paul na Ruby)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *