Mchipuko

Yammi, Msanii wa Nandy azidi Kutamba | Nakuchukia ya trend kwenye Youtube

Baada ya utambulisho wake, yammi ameonekana kuvutia watu wengi sana na nyimbo zake zimeanza kupata umaarufu. Huyu atakuwa msanii wa kwanza kwenye label ya African princess inayomilikiwa na Nandy.

Wengi wamefurahishwa sana na hatua ya Nandy kwa bidii yake sanasana kujitolea kuwasaidia wanamziki wa kike kwani alisema kuwa lebo yake itakuwa ni ya wasanii wa kike wenye talanta na hawajui kwa kwenda.

Katika uzinduzi wa Msanii huyu, Nandy aliweza kuwaalika wasanii tajika wa kike kutoka nchi ya Tanzania kama vile, Gigy Money, Lady jaydee na wengineo. Kila aliyepata nafasi ya kuongelea msanii huyu alionekana kumsifu kwa uwezo wake wa kuandika na kuimba.

Yammi Kufananishwa na Zuchu.

Yammi na zuchu

Kwa wale wataalam wa mziki wanaamini Kwamba kuna ufananisho wa msanii huyu na Zuchu kwani sauti iko palepale na pia yasemekana Yammi ametokea Zanzibar Ambapo pia ni Nyumbani mwa msanii Zuchu.

Uwezo wake wa Kuimba Live pia unafananishwa na Zuchu bila kusahau sauti yake ya kukwaruza kama ile ile ya Zuchu. Nandy alipooulizwa kama Yammi ametokea Zanzibar alikataa na kusema kuwa msanii wake ni wa Dar es salam. Aliongeza kusema haoni chochote cha kulinganisha Yammi na Zuchu kwani kila msanii ana uwezo wake na mafans wake

Nyimbo mpya za Yammi

Baada ya kuzinduliwa, Yammi aliachia nyimbo tatu ambazo ni;

  1. Namchukia – Yammi
  2. Tunapendezana – Yammi
  3. Hanipendi – yammi

Nyimbo hizi tatu zipo kwenye Ep yake inayojulikana kama Three hearts yenye nyimbo tatu. Yammi pia aliachia video ya Namchukia ambayo kwa sasa tarehe 23 January 2023, iko na views zaidi ya milioni. Kumbuka video hii ina siku tatu baada ya Kuachiwa.

Picha za Yammi Msanii wa Nandy

Picha za Yammi

Kwa sasa picha za Yammi zimeanza kuzunguka kwenye mitandao na kusema kweli manamziki huyu anapendeza kwa maumbile. Nguo aliyoivaa kwezi uzinduzi wa Ep yake ilimpendaza zaidi na iliendana kabisa na shepu yake.

Pia soma, Nandy alivyokutana na Billnass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *