MaishaMchipuko

Zuchu na diamond platnumz wafunguka kuhusu uhusiano wao

Kwa wiki kadhaa, habari iliogonga vichwa vya habari ilikuwa kuhusiana na ukaribu wa zuchu na diamond platnumz. Wengi walikisia kwamba wawili hawa walikuwa wakipanga kufunga ndoa.

Media nazo hazikuachwa nyuma kwa kisambaza habari hizo ambapo wasafi media ilishikilia nafasi ya kwanza kiongelea uhusiano wa diamond platnumz na Zuchu.

Ilisemekana wawili hawa walitarajiwa kufunga pingu za maisha mnano February tarehe 14, siku ya wapendanao duniani. Hii haikufanyika badala yake, zuchu aliandaa tamasha kubwa kwa jina mahaba ndindindi.

Kwenye red carpet, zuchu na diamond walionekana pamoja ila walipoukizwa kama wako kwenye uhusiano wa kimapenzi, walikataa huku kila mmoja alijitetea kivyake. Kwa upande wake, diamond platnumz alisema Zuchu ni mwanawe na uhusiano wake ni wa kikazi tu.

Zuchu pia alirudia maneno hayo hayo huku akiongezea kwamba hata diamond platnumz anamfahamu mpenzi wa zuchu ambaye Yuko Nje ya nchi. Diamond pia alitangaza kuwa kwenye uhusiano na mpenzi mpya huku akimtumia jumbe za valentine “Live” kwenye interview.

Swali letu ni, mbona wawili hawa waliamua kueneza haya maneno ya uhusiano wao huku wakijua sio kweli?, Je tuwalaumu diamond platnumz na Zuchu ama media za Tanzania?

Ni hayo tu kwa sasa kuhusiana na uhusiano wa zuchu na diamond platnumz. Zidi kutegea habari zetu zisizo tegemea upande wowote.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *