Sanaa

Waigizaji wa Pete Maisha magic na majina yao kamili

  • Waigizaji wa Pete Maisha magic na majina yao kamili
  • Ni tamthilia inayopeperushwa ndani ya maisha magic na maisha magic plus
  • Tamthilia ya pete imetayarishwa na Daudi Anguka
  • Pete Maisha magic ina wahusika zaidi ya sitini
  • Leon Ongaya ambaye kwa tamthilia ya pete anajulikana kama Kiongozi Mbura alipata tuzo ya msanii bora katika kitengo cha drama kwenye tuzo za kalasha awards 2020

Ni kati ya zile tamthilia zinazopendwa zaidi ndani ya maisha magic East na maisha magic plus. Tamthilia ya pete inaangazia vijana wawili wanaong’ang’ania uongozi wa kisiwa baada ya baba yao kufariki kabla hajataja mridhi wake. Tamthilia hii inaangazia mapenzi na uongozi katika jamii ya kisiwa cha funzi.  Mwandishi mkuu katika tamthilia hii anajulikana kama Yusuf dalu mtayarishi mkuu akiwa Daudi Anguka.

Waigizaji wa pete maisha magic na majina yao kamili

  1. Mutran tamim             – Jasiri
  2. Leon Ongaya               – mbura
  3. Aisha Mwajumlah      – Nimimi
  4. Selestine Nyagha       –    Nuru
  5. Sophie Reuben           – Safira
  6. Sahara Mohammed – Karembo
  7. Susan Kadide              – Bi. Komo
  8. Ali Shahibu                   – Sudi
  9. Abdallah Bakari          – Kalume
  10. Hillary Namanje          – Kiza
  11. Juma Mwatseka         – Bundez
  12. Olivia makena             – Sitara
  13. Gillie Owino                  – Msiri
  14. Rehema Rajab            – Jinale

Mutran Tamim | Jasiri

Jasiri Pete Maisha Magic - mutran tamim

Ni kijana jasiri kama jina lake na ni mtu anayependa kutetea haki ya wanakisiwa. Mutran Tamim ni mzaliwa wa nchi ya tanzania na hii ndio tamthilia yake ya kwanza kuigiza hapa nchini kenya. Kulingana na tamthilia ya pete, Jasiri ni mtoto wa marehemu dalu aliyekuwa kiongozi wa funzi kabla ya kuaga dunia. Babake dalu alikuwa amempendekeza ili kuridhi uongozi wake ila kwa tamaa, kakake alikataa na kuwa kiongozi kinyume na chaguo la babake na mizimu. Baada ya Mbura kusafiri kisiwa jirani kumfuata mke wake nimimi, Jasiri aliapishwa kama kiongozi baada aliyekuwa kaimu, mzee kiza kung’atuliwa uongozini na wana kisiwa.

Kiongozi Mbura | Leon Ongaya

Kiongozi Mbura pete maisha magic - Leon Ongaya

Wengi wanamfahamu kama kiongozi katili mwenye hana huruma na wanakisiwa wenzake. Mbura ni mpenzi wake nimimi ila bado hawajaoana rasmi. Alipopata uongozi, Mbura alipandisha kodi ya kila kitu na maisha yakawa magumu kwa wana kisiwa wa funzi. Mbura haelewani na kakake jasiri kwani anasema babake alimpendelea sana jasiri. wakati wakiwa wadogo, Mbura aliamua kutoendelea na masomo ili jasiri aweze kuendelea na masomo.

Nimimi | Aisha Mwajumlah

Nimimi Pete Maisha magic - aisha Mwajumlah

Ni mwanmke mrembo anayependa bwanake hata kama bwanake ni katili. Nimimi hupenda maelewano na hujaribu sana kuwaongelesha Mbura na jasiri ili waweze kulelewana. Japo anatoka kwa familia tajiri, Nimimi aliamua kuja funzi kuishi na Mbura tena akanunua nyumba ili wawili hawa waishi pamoja. Nimimi ashawahi pigwa sana na mpenzi wake Mbura lakini bado amebaki na yeye. Baada ya kurudishwa kwao na Mfalme Zurui kwa njia ya kutekwa nyara, Nimimi bado alibakia na msimamo uleule kwamba hataolewa na yeyote yule hata kama ni mtoto wa mfalme isipokuwa Mbura.

Nuru | Selestine Nyagha

Nuru pete Maisha magic - Selestine Nyagha

Ni msichana mrembo sana japo hana bahati na mapenzi. Humpenda jasiri na huamini siku moja wawili hawa watakuja oana. Mapenzi yake na jasiri haishi vituko kwani kunaye safira (kitunusi) ambaye pia anapigania kuwa na jasiri. Nuru ni mjukuu wa bi komo na Bi. Komo ni yeye amekuwa akimulea baada ya mamake Nuru kuaga dunia. Nyanyake ambaye ni Bi. Komo hutaka Nuru aolewe na jasiri ila ni lazima Jasiri amtolee Mahari Mjukuu wake kabla ya kumchukua kama mke wake.

Safira | Sophie Reuben

Safira pete Maisha Magic - Sophie Reuben

Safira ni kitunusi aliyetumwa kisiwani ili kufuata pete na malkia wake. Majina yake kamili ni Sophie Reuben. Baada ya safira kuingia kisiwani, alianza urafiki na jasiri na baadae kusahau alichotumwa na kuwa mpenzi wake jasiri. Safira ni mpinzani wake Nuru na wote wawili wanapigania jasiri. Kumbuka Safira sio binadamu ila yeye ni mmoja wa familia ya Vitunusi wanaosemekana kuishi bahari. Kulingana na tamthilia ya pete, Familia ya Vitunushi waliwahi kupigana na wanakisiwa wa funzi na hapo ndipo walipoteza pete yao ndio maana mpaka wa leo wanajaribu kuifuatilia.

Karembo | Sahara Mohammed

Karembo pete maisha magic - Sahara Mohammed

Ni msichana mcheshi na kawaida yake hupenda kucheka kila kitu hata kama mtu apo karibu na kufa. Hufanya kazi kwa kasri na aliwahi kumpokonya nimimi mumewe Mbura. Hupenda wanaume wenye sifa za pesa na Uongozi. Huwa hampendi kalume maana hana pesa na pia hana sifa za uongozi. Mpaka wa leo bado anamtaka Mbura awe mume wake lakini Mbura moyo wake uko kwa Nimimi.

Bi. Komo | Susan Kadide

Bi komo pete maisha magic - Susan Kadide

Bi.Komo Majina yake kamili ni Susan Kadide, Ni kati ya wale wanakisiwa wakongwe wanaoelewa historia ya kisiwa cha funzi. Bi komo ni mama anayeishi na Nuru kama mjukuu wake. Bi komo ana siri nyingi za kisiwa cha Funzi na mara kwa mara hufuatwa na wazee wa kisiwa ili kuwapa mawaidha. Bi komo huwa sio muoga na hupenda kusema vitu peupe peupe. Kazi yake huwa ni kuwashonea wanakijiji mikeka.

Sitara | Olivia Makena

Sitara Pete Maisha Magic - Olivia Makena

Ni mtoto mdogo aliyeokotwa baharani baada ya ajali ya mashua. Sitara alichukuliwa na Marehemu Mzee dalu na kuamua kumlea kama babake. Sitara amepitia mengi sana kwenye kasri kwani Kiongozi Mbura alikuwa hampendi hata Kidogo. Aliyekuwa akimjali mtoto huyu ni nimimi kwani hata Karembo ambaye ni mfanyi kazi hampendi sitara. Ashawahi kujaribu kujitoa uhai ila aliokolewa na Jasiri pamoja na Nuru.

Sudi | Ali Shahibu

Sudi pete Maisha magic - Ali Shahibu

Kama kuna mwanaume mbea  kisiwani funzi basi ni huyu bwana sudi. Sudi ni kijana mcheshi na kila ukimuona kwa runinga lazima utacheka hata kabla hajatamka chochote. Watu humpenda sana sudi na akikosekana naona mafans wake hawatalala. Sudi hufanya kazi kwa kasri la kiongozi na mpaka leo kwake hakujajulikana. yaani hakuna anayejua sudi anaishi wapi. Ni rafiki yake Kalume na wote wanapatikana mitaani tu kusambaza umbea.

Kalume | Abdallah Bakari

Kalume maisha magic - Abdalla Bakari

Kalume ni mtoto wa mzee kiza. Kwa majina kamili anajulikana kama Abdallah Bakari. Huwa hana kazi maalum ila wakati mwingi huwa ako ufuoni kuvua samaki. Kalume anampenda sana karembo ila mpaka wa leo wawili hawa hawajawahi kuishi pamoja kwani chaguo la karembo sio Kalume. Aliwahi kupelekwa masomoni nje ya kisiwa cha funzi ila akatumia karo ya shule kwa kuponda raha na wanawake na kurudi kisiwani bila chochote.

Kiza | Hillary Namanje

Mzee kiza pete maisha magic - Hillary Namanje

Ni mzee wa baraza la wazee kisiwani Funzi. Kiza ni babake kalume na pia kwa sasa imejulikana kiza ni Babake Mbura. Kiza ni mzee anayependa kupinga kila kitu hata kama kina manufaa kwa kisiwa. Aliwahi kuachwa na Mbura kama kaimu kiongozi na akaponda mali ya kisiwa huku akitaka kuiuza ardhi ya shule bila kujali penye watoto watasomea ama kucheza. baada ya kuachiwa uongozi wa funzi alimchukua bi Jinale kama malkia wake. Baada ya mda vijana waliungana na kumtoa uongozini na hapo ndipo jasiri akachaguliwa kama kiongozi.

Msiri | Gillie Owino

Msiri pete maisha magic - Gillie Owino

Ni mzee wa kisiwa anayesemekana kuwa na maarifa mengi. Baada ya Mzee Dalu kuaga, Msiri aliachiwa jukumu ya kuendesha kisiwa na kuwapa mawaidha viongozi jinsi ya kuongoza kisiwa. Yeye ni mshauri mkubwa na ndiye ana uwezo pekee wa kuongea na Mizimu. Ni mmoja wa wazee wa baraza la funzi na pia yeye ndiye huapisha viongozi na kuwapa ushauri.

Bundez | Juma mwatseka

Bundez pete maisha magic - Juma Mwatseka

Bundez majina yake kamili ni Juma Mwatseka. Ni mmoja katika baraza la wazee. Bundez pia ni baba mlezi wa karembo aliyemchukua baada ya mamake karembo kuaga dunia. Bundez ni mzee mwenye masifa chungu nzima. Yeye na mzee kiza huwa hawaeleweni maana kila mmoja anapenda kupinga mwingine sanasana wakiwa katika baraza la wazee.

Soma hii pia ( Waigizaji wa Maria citizen tv na majina yao kamili)

 

 

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *