Upishi

Jinsi ya kupika pilau

Ni chakula nikachosifika Ila wengi hawana ufahamu wa kupika hiki chakula kitamu. Pilau ni chakula chenye hutumika sana kwenye sherehe ambapo sherehe yenye Haina pilau huonekana Kama haijakamilika. Wengi wameweza kuzungumuzia jinsi ya kupika pilau huku wengi wao wakiamua kutengeneza video ili kuonyesha uwezo wao katika sekta ya upishi.

Jinsi ya kupika pilau Kama hauna uzoefu

Iwe watumia nyama au kuku, mwisho wa kusoma maelekezo haya utafahamu kupika pilau na bila shaka utakuwa hodari. Kabla ya maelezo zaidi, unahitaji vifuatazo

  • Mchele (rice Kama vikombe vitatu
  • Nyama (meat nusu kilo
  • Vitunguu maji (onions Kama tatu
  • Viazi mbatata (potatoes pia tatu
  • Vitunguu swaum (garlic cloves nne
  • Tangawizi iliyosagwa (ginger
  • Hiliki
  • Karafuu
  • Pilipili mtama
  • Mafuta
  • Nyanya
  • Chumvi
  • Limao

Katakata nyama, tia limau Kisha uichemshe mpaka iive kabisa alafu uieke pembeni. loweka mchele kwa mda wa dakika kumi. Chemsha maji pia ueke kando. Katakata vitunguu na viazi Kisha ueke kando.Wekelea sufuria kwa Moto Kisha eka mafuta.

Mafuta yakishika Moto, tia vitunguu alafu acha kwa Moto mpaka ziwe rangi ya kahawa. Tia nyama kwa huo mchanganyiko alafu Pika mpaka zigeuke rangi ya brown. Baada ya hapo tia kitunguu swaum na tangawizi alafu acha huo mchanganyiko kwa Moto kwa mda wa dakika mbili.

Jinsi ya kupika pilau

Baada ya dakika mbili tia binzare nyembamba, hiliki, amdalasini, pilipili mtama. Baada ya hapo zidi kugeuzageuza huu mchanganyiko kwa mda na ikishikana vizuri tia mchele na uzidi kukoroga Ila punguza Moto ili kuzuia kuungua. Baada ya hapo tia maji ya kutosha na chumvi Kisha funika. Maji yakishakauka geuzageuza Tena mchanganyiko huo Kisha funika Tena alafu uache kwa Moto mpaka iive kabisa.

Baada ya hapo tengeneza kachumbari kwa kutumia nyanya, kitunguu maji na hoho Kisha tia chumvi na limau. Pakua pilau yako na ufurahie utamu usiokuwa na kifani. Maelezo ya jinsi ya kupika pilau imeletwa kwako na mwangaza

 

 

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *