Upishi

Jinsi ya kupika chapati kitamu chenye radha

MAHITAJI YA JINSI KUPIKA CHAPATI

Japo kuna maelezo mengi ndani ya youtube na facebook  na kwenye mitandao jinsi ya kupika chapati, nimechukua mda ili kuwapa njia mwafaka ya upishi wa chapati. Wengi wana uzoefu ila sio wengi wanaoelewa kabisa upishi huu. Yafuatayo ni maelezo  na natumai yatakusaidia

Unga wa ngano vikombe 5
Samli ilioekwa motoni Kwa sekunde kadhaa vijiko vya mezani 3_4
Chumvi kiasi chako
Maji yasiokuwa moto wala baridi(at room temperature) glass 2 ndogo.

MATAYARISHO YA JINSI YA KUPIKA CHAPATI

Weka unga kwenye bakuli uchanganye na chumvi vizuri
Weka samli uchanganye mpaka vidonge vyote viishe
Weka maji kidogo kidogo ukiendelea kukanda unga mpaka ushikane na ulainike vizuri.
Funika unga kisha ueke pembeni Kwa takriban dakika 30(ukieka Kwa muda mrefu zaidi ndio utalainika zaidi)
Funua unga wako utoe madonge matatu(size ya madonge itategemea na mahali pako pa kusukuma. Kama ni pakubwa unaweza hata ukafanya donge moja Tu)
Sukuma donge moja moja kama chapati kisha upake mafuta na ukunje kama swissroll(kufanya tabaki)
Gawanya size unayotaka na ukunje vizuri chapati zako
Ziwache tena Kwa takriban nusu saa au zaidi ili zizidi kulainika
Bandika chuma cha kuchomea chapati motoni na uache kishike moto
Chuma kikiendelea kushika moto, sukuma chapati zako size unayotaka (zisiwe nene wala nyembamba Sana)
Chuma kikishashika moto, weka chapati uanze kuchoma
Chapati ikishika rangi kidogo upande mmoja,geuza upande wa pili pia ishike rangi
Weka samli upande mmoja na uipike chapati Kwa sekunde kadhaa huku ukiemezea chini Kwa kitambara au kijiko kikubwa ili ikolee rangi nzuri. Geuza upande wa pili ufanye vivyo hivyo.
Chapati zipo tayari
Andaa zikiwa moto kwa maini, maharagwe au chochote upendacho.

MAELEZO YA ZIADA YA KUPIKA CHAPATI

Ongeza unga wa maziwa takriban vijiko 3_4 vya mezani itasaidia chapati kuwa laini zaidi
Weka chapati kwenye mfuko wa lailoni ili zisipoe na pia zibaki laini
Usiiwache chapati Kwa muda mrefu kwenye moto kwasababu itakuwa kavu
Usipike chapati Kwa Moto mkubwa Sana kwasababu itaungua kabla ya kuiva.
Usiwache wazi madonge yako ya chapati au unga baada ya kuukanda kwasababu unaweza ukafanya ukoko juu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *