Afya

Kenya yatoa wito wa usawa katika usambazwaji chanjo ya corona

Kenya yatoa wito wa usawa katika usambazwaji chanjo ya corona
Kenya imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuhimiza upatikanaji sawa wa chanjo ya COVID-19 au corona kufuatia taarifa za mafanikio katika majariibio ya chanjo.

Patrick Amoth, mkurugenzi mkuu wa afya katika Wizara ya Afya ya Kenya amesema Kenya inakaribisha tangazo hilo la mafanikio ya chanjo iliyo salama, ambayo itaharakisha juhudi za kudhibiti janga la corona

Amesisitiza kuwa chanjo ya COVID-19 ni bidhaa ya afya ya umma duniani ambayo nchi zote zinapaswa kuipata kwa usawa. Pia amethibitisha tena uungaji mkono wa Kenya kwa WHO kama shirika maalumu la Umoja wa Mataifa linaloratibu afya ya dunia na dharura za afya duniani.

Amoth amesema Kenya, chini ya usimamizi wa kamati ya kitaifa ya COVID-19 inatekeleza mikakati ya kina inayolenga kukabiliana na kuenea kwa COVID-19.

Mnamo Jumatatu, Novemba 9, 2020 kampuni za kutengeneza dawa za Pfizer na BioNTech zilisema chanjo hiyo mpya imebainika kuwa na asilimia 90 ya uwezo wa kutibu. Hii ina manaa kuwa tisa kati ya wagonjwa 10 wa Covid-19 waliotumia chanjo hiyo walipata afueni.

Kampuni hizo pia zilisema kuwa dawa hiyo haikuonyesha madhara yoyote kwa wagonjwa waliotumiwa kuifanyia majaribio.
Chanzo: https://parstoday.com/sw

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *