MchipukoSiasa

Mpinzani wa Rais Meseveni, Bobi Wine atiwa mbaroni tena

Mpinzani wa Rais Meseveni, Bobi Wine atiwa mbaroni tena; IGP ataja sababu
Kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP) na mgombea urais nchini Uganda, Robert Kyagulanyi, maarufu kwa jina la Bobi Wine amekamatwa tena mapema leo na polisi, akiwa katika harakati zake za kufanya kampeni.

Mbunge huyo wa Kyadondo Mashariki, amekamatwa kufuatia mzozo kati ya wafuasi wake na watendaji wa usalama katika eneo lake la kampeni.
Imeelezwa kuwa kukamatwa kwa Bobi Wine, kumekuja baada ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo IGP Martin Okoth Ochola, kumuonya kwamba amekuwa akikaidi miongozo ya uchaguzi yenye nia ya kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa wa COVID-19.

“Licha ya maonyo yanayotolewa mara kwa mara kwa wagombea, mawakala wao na umma kwa ujumla juu ya athari mbaya na hatari za kiafya za kufanya mikutano na maandamano yasiyoruhusiwa, tunaendelea kushuhudia vitendo vya kukaidi na kupuuza kabisa miongozo ya Tume ya Uchaguzi EC, kwa hivyo wale watakaokaidi miongozo hii watawajibishwa” amesema Mkuuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda.

bobi wine arrested
Hii si mara ya kwanza kwa mwanasiasa huyo machachari wa upinzani kutiwa mbaroni, kwani amekuwa akikamatwa mara kwa mara kwa sababu mbalimbali.
Zaidi ya wagombea 10 wamepasishwa kuwania kiti cha rais nchini Uganda akiwemo kamanda wa zamani wa Jeshi, Mugisha Muntu na aliyekuwa Waziri wa Usalama Jenerali Henry Tumukunde.

Wagombea hawa watachuana na Rais Yoweri Kaguta Museveni mwenye umri wa miaka 76 ambaye anaiongoza Uganda kwa zaidi ya miaka 30. Mwaka 2017 Bunge la Uganda lilipiga kura ya kuondoa ukomo wa umri wa miaka 75, na kumtengenezea Museveni ambaye sasa ana umri wa miaka 76, njia ya kuwania urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mapema mwakani.

Soma hii pia(najuata kuachana na Zari, diamond Platnumz asema

CHANZO: https://parstoday.com/sw

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *