Maisha

SWALA YA JANAZA

SWALA YA JANAZA

wengi wetu hatujuwi kumswalia maiti. Haswa tukishamfikisha msikiti utakuta wengi watoka baada ya swala ya kipidi alichofikia. Sio kuwa watoka hataki kumswalia maiti Bali ni kuwa hajuwi atasoma nini katika takbira zile nne.

Leo naomba niwajuze japo uchache naojuwa Mimi nakama Kuna mahali nitakosea naomba munirekebishe.

Swala ya JANAZA ina Takbir 4 tu.
Atakaeswali Swala ya Maiti, hufutiwa madhambi mfano wa Jabal Tuur.

Takbiri ya Kwanza

Unasoma Suratul Fatiha tu.

Takbiri ya Pili

Unamswalia Mtume Sal’Allahu Alaihi wa Sallam kama unavyomsalia katika swalah nyengine.

Takbiri ya Tatu

Kumuombea Maiti dua, kiufupi utasema :- “Allahumma’ghfirlahuu, War’hamhuu wa Aafihi wa’af-anhuu.
Allahumma In kaana Muhsinan, Fazid Ihsanihii, Wa In kaana Musii’an Fatajaawaz Anhu.”

Takbiri ya Nne

Utasoma “Allahumma Laa Tahrimnaa Ajrahuu, wa Laa Taftinnaa Baadahuu, Wa’ghfirlanaa Wa Lahuu”

Kisha unatoe Salamu kama kawaida.
Watumie wengine ili wapate fadhila za kumswalia maiti na tuhimizane kujitaahid kuswali Swalaatul Janaaza kila itokeapo.

*Allah atupe Husnul Khaatimah indal Maut, Amin.*

Soma hii pia ( jinsi ya kuoga janaba)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *