Mchipuko

Diamond platnumz asema anajuta kuachana na Zari

Diamond platnumz asema anajuta kuachana na Zari kwa maana alichangia pakubwa katika maisha yake

Uhusiano wa kimapenzi wa staa wa bongo Diamond Platnumz umekuwa kwenye vichwa vya wanamitandao kila kuchao, huku akianza na uhusiano kati yake na Wema Sepetu ambapo alimtambulisha kwa mashabiki huku baadaye wakiachana.

Baada ya wawili hao kutengana, Diamond alimpenda Zari Hassan ambaye amemzalia watoto wawili, kisha Hamisa Mobetto huku akija Kenya na kumpenda mwanamuziki Tanasha Donna baada ya kubarikiwa na mtoto mmoja wakaachana.

Akiwa kwenye mahojiano, Diamond alisema kuwa anajuta kuachana na baby mama wake Zari Hassan, maneno yake yanajiri wakati pale Zari na wanawe wawili walienda kumuona Tanzania.

Huku akizungumzia kwa nini anajuta alisema kwamba Zari alimsaidia awezavyo katika kukuza usanii na muziki wake.

“Naeza sema leo kwa mara ya kwanza kuwa, kwa wanadada wote ambao nimewai kuwa nao katika mahusiano hasa wenye wamenizalia, huwaga najutia kuachana na mmoja wao ambaye ni Zari. Kusema kweli Zari alichangia katika mafanikio yangu ya muziki na maisha kwa ujumla,” Simba Alizungumza.

Soma hii pia ( IMEI wa Zari Hassan wazua gumzo)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *