Maisha

HII NDIO DAWA YA MKE ASOPENDA NDUGU WA MUME

HII NDIO DAWA YA MKE ASOPENDA NDUGU WA MUME

Siku moja wakiwa wamekaa pamoja mume pamoja na mke wake, mume akamwambia mke wake…

“Mke wangu nimewakumbuka sana ndugu zangu (kaka zangu dada zangu na hata baba na mama) tujumuike pamoja na kula pamoja

Kesho nitawaalika ili tujumuike nao katika chakula cha mchana, itabidi uandae chakula kwa ajili yao.”

Mke akasema kwa unyonge “sawa mungu akipenda.”

Asubuhi ya siku iliyofuata mume akatoka kwenda katika mishughuliko yake lakini baada ya masaa kadhaa akarejea nyumban na kumuuliza mke wake.

“Mke wangu umeandaa chakula cha mchana kwa ajili ya wageni? maana baada ya lisaa limoja watakuwa wameshafika.”

Mke akajibu “hapana sijapika kwani ndugu zako sio wageni hapa watakula chochote watakachokikuta.”

Mumewe akamwambia mungu akusamehe mke wang kwa nini unayasema hayo ilihali tokea jana nilikuambia ya kuwa wazazi wangu wanakuja

Na kwa nini hukunambia mapema kuwa hutopika ilihali baada ya lisaa limoja wazazi wangu watakuwa hapa nini unafanya mke wangu.”

Mke akamjibu “waache waaje nitawataka radhi, kwani wao si wageni hapa watakula chochote watakachokikuta.”

Basi mume ikambidi aondoke pale nyumban kwa kukwepa fedheha.

Baada ya dakika kadhaa mlango ukagongwa mke akaenda kuufungua…

Kwa mshangao mkubwa alipofungua mlango akakuta wageni waliokuja hapo ni wazazi wake babaake, mamaake dada zake pamoja na kaka zake

Akastuka kwa mshangao na kuwakaribisha ndani,

Baba akamuuliza kuwa mume wake yupo wapi?

Akajibu kuwa alikuwepo hapa ametoka dakika chache kabla hamjafika.

Baba akamwambia “mumeo jana alitupa taarifa kuwa leo anatuarika hapa tuje kula pamoja chakula cha mchana sasa vipi yeye ametoka si busara.”

Yule mwanamke akastuka kwa taarifa hiyo na kuanza kujifikicha mikono yake huku akiipiga piga hali ya kuchanganyikiwa.”

Ikambidi aingie ndani na kumpigia simu mume wake akamwambia “kwa nini hukuniambia kuwa wazazi wangu ndio wanaokuja?”

Mumewe akamjibu “Wazazi wangu na wazazi wako wote ni kitu kimoja/hawana tofauti.”

Mke akamwambia “Lete chakula huku chakula kilichokuwepo ni kichache haki tawatosheleza.”

Mume akamjibu “Mimi nipo mbali na hao si wageni watakula chochote kilichopo kama wewe ulivyokuwa ukitaka kuwalisha wazazi wangu.”

Shea ujumbe huu kadri uwezavyo

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *