Siasa

Magufuli akabidhiwa cheti cha ushindi

Magufuli akabidhiwa cheti cha ushindi; aahidi kuwatumikia Watanzania wote
Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli hatimaye amepokea cheti cha ushindi wake katika uchaguzi wa urais ulikamilika matokeo yake.

Jaji mstaafu na mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Semistocles Kaijage aliwakabidhi rais Magufuli na makamu wake Samia Hassan Suluhu vyeti hivyo kufuatia ushindi mkubwa wa chama tawala cha CCM, uchaguzi ambao umepingwa na vyama vikuu vya upinzani.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa cheti hicho, rais Magufuli amesema kwamba ushindi alioupata ni deni kubwa kwa Watanzania huku akiwashukuru wapinzani wake kwa kumpatia ushindani mkubwa.

Kiongozi huyo amesema kwamba upinzani huo umesaidia katika kufahamu ni nini Watanzania wanataka.

”Nawashukuru pia na kuwapongeza kwa kukubali matokeo na kuja kushiriki hafla hii. Hii ni ishara ya kukomaa kwenu kisiasa – hongereni sana”.

Tundu Lissu mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Chadema alipozungumza na waandishi wa habari na kutangaza kupinga matokeo ya uchaguzi

Bwana Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kukipa ushindi chama chake cha Mapinduzi (CCM) katika nafasi ya Urais, Ubunge na kule Zanzibar katika nafasi ya uwakilishi na nafasi ya Udiwani.

”Kupata asilimia 84.4 ni imani kubwa sana kwa Watanzania na nasema kwa dhati nina deni kubwa sana kwa Watanzania, imani yao nitaitimiza kwa kufanya kazi sana usiku na mchana”, Bwana Magufuli amesema.

“Siasa sio vita siasa sio ugomvi sisi sote ni Watanzania napenda kuwaahidi nitashirikiana nanyi katika kuhakikisha tunasukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Tanzania kwanza mambo mengine baadae” Magufuli amesema.

Hayo yanajiri wakati ambao vyama vya upinzani nchini Tanzania vya CHADEMA na ACT Wazalendo vimesema kuwa havitambui matokeo ya uchaguzi. Vyama hivyo vimeitisha maandamano hapo kesho.

Soma hii pia ( sina ugomvi na Nandy ; zuchu)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *