MzikiSanaa

SINA UGOMVI NA NANDY, ZUCHU ASEMA

SINA UGOMVI NA NANDY, ZUCHU ASEMA

Zuchu amefunguka kuhusu kuwa na bifu na mwimbaji mwenzie Nandy

Nandy
Nandy

Zuchu amesema kuwa yeye na Nandy hawajawahi kuwa na tatizo na wala hawana tatizo lolote, ila kinachotokea ni watu tu kuwashindanisha.

“Hata Kipindi natoa EP yangu Nandy aliipost, huwezi kuzuia watu kukushindanisha, kwasababu watakushindanisha tu, lakini nachukia maneno ya watu wanaosema natengenezwa kumshusha Nandy,” amesema Zuchu kwenye mahojiano na WasafiFm Ijumaa hii.

Zuchu
Zuchu

Pia Zuchu ameongelea maneno yanayodai kuwa anatengenezwa ili kumshusha msanii mwenzake #Nandy, na kusema maneno hayo yanaongelewa na watu wasio na mapenzi mema kwake ili tu kumtengenezea maadui ambao yeye hawaitaji.

“Nandy ni msanii mzuri na anafanya mambo yake, na mimi natafuta ridhiki yangu ” amesema Zuchu.

Soma hii pia ( uhusiano wa Zuchu na diamond platnumz)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *