Sanaa

Uhusiano wa Zuchu na diamond platnumz

Zuchu na diamond platnumz wamekuwa na ukaribu mkubwa sana kwa mda. Wengi wameanza kuwashuku wawili hawa. Kwa mda sasa, diamond platnumz amekuwa akiifuatilia kazi ya Zuchu na kuifanyia matangazo kuliko kazi za wasanii wengine wa wasafi.

Kumbuka wasafi ama ukipenda WCB Kuna wasanii wengine Kama vile Rayvanny, Mbosso na Lavalava. Watatu hawa wanaonekana kuwekwa kando na anayeshughulikiwa kwa Sasa ni msanii zuchu. Je, sababu ya Diamond Platnumz kufanya haya Ni kwa sababu gani?

View this post on Instagram

E &M WEDDING RECEPTION ? ? @lukambaofficial

A post shared by DIAMOND PLATNUMZ ? (@diamondplatnumzfamily) on

Kulingana na utafiti wetu Ni kuwa. Kwa Sasa, Zuchu ako na wafuasi wengi sana na kazi zake tayari zimeanza kuingizia kampuni ya wasafi hela ndefu. Kama biashara ya Aina yoyote, lazima mwanabiashara atengeneze faida kwa kila biashara. Mwanabiashara akiona bidhaa flani inaingiza hela nyingi, basi huamua kuongeza stock ya hiyo bidhaa ili kujiongezea mapato.

Wengi wanaodhania kuwa wawili hao Wana uhusiano wa kimapenzi mjue sio kweli kwani wawili hawa wako kwenye uhusiano wa biashara. Zuchu na diamond platnumz huenda wakatengeza hela sana wakiendelea na moyo huohuo wa kufanya kazi pamoja.

Diamond Platnumz na Zuchu

Kwa Sasa tunazidi kufuatilia maoni ya wasanii wengine wa wasafi watakachokisema. Haijajulikana Kama wanaridhika na hali inayoendelea Ila hapa mwangaza news tutazidi kuwajuza mengi kadri ya uwezo wetu.

(Tazama picha za mwanamke anayesemekana kuwa mpenzi wa diamond platnumz)

Loading

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *